Pata taarifa kuu
ANGOLA-UCHAGUZI

Uchaguzi nchini Angola: Joao Lourenço, mrithi wa Dos Santos

Nchini Angola,baada ya kupata zaidi ya 64% ya kura, chama cha MPLA kimeshinda uchaguzi, kwa mujibu wa takwimu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Lakini baada ya miaka 38 madarakani, rais Dos Santos aliamua kuachia ngazi na kumkabidhi Joao Lourenco kijiti cha kuwania kwenye kinyang'anyiro cha urais.

Joao Lourenço katika mkutano na waandishi wa habari mjini Luanda tarehe 22 Agosti 2017.
Joao Lourenço katika mkutano na waandishi wa habari mjini Luanda tarehe 22 Agosti 2017. REUTERS/Stephen Eisenhammer
Matangazo ya kibiashara

Bw. Lourenço ni Waziri wake wa Ulinzi, ambaye atachukua uongozi wa nchi hiyo. Bw. Lourenco ni mmoja wa makad wakuu wa chma cha MPLA.

Bw Lourenço mwenyewe alikumbusha mnamo mwezi Februari, wakati aliteuliwa rasmi kupeperusha bendera ya chama cha MPLA katika Uchaguzi Mkuu nchini Angola.

"Ni kwa muda mrefu nikijiandaa kwenye nafasi hii na nikiandaliwa. Mimi ni mmoja wa makada wakuu wa chama cha MPLA kwa miaka mingi, "alisema Joao Lourenço.

Joao Lourenço alizaliwa mwaka 1954 katika mji wa Lobito magharibi mwa Angola, na ni mshirika wa karibu wa miaka mingi wa Jose Eduardo dos Santos. Kama mtangulizi wake Bw. Lourenco alisomea katika nchi ya Urusi ( ya zamani)Alijiunga na jeshi mwaka 1974, alipigania uhuru wa Angola. Miaka kumi baadaye, kazi yakelichukua mwelekeo wa kisiasa.Afisa huyu wa jeshi katika ngazi ya juu aliteuliwa kuwa gavana na alianza kujiunga na chama cha MPLA. Alikua mkuu wa kitengo cha kisiasa wa tawi la zamani la kijeshi la cha MPLA na makamu wa Spika wa Bunge.

"Agenda ya Serikali ya mwaka 2017-2022: Kuboresha ni vizuri, kusahihisha ni mabaya," bango kutoka makao makuu ya MPLA, chama cha rais.
"Agenda ya Serikali ya mwaka 2017-2022: Kuboresha ni vizuri, kusahihisha ni mabaya," bango kutoka makao makuu ya MPLA, chama cha rais. RFI/Sonia Rolley

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.