Pata taarifa kuu
SEMENYA

Caster Semenya awasilisha rufaa nyingine katika mahakama ya Uswis

Bingwa wa mbizo za mita 800 raia wa Afrika Kusini, Caster Semenya amewasilisha rufaa nyingine katika mahakama kuu ya Uswis, akipinga kushindwa katika kesi ya kuamua kuhusu kiwango cha homoni mwilini mwake.

Mwanariadha wa Afrika Kusini, Caster Semenya akishangilia ushindi katika moja ya mbio alizoshiriki
Mwanariadha wa Afrika Kusini, Caster Semenya akishangilia ushindi katika moja ya mbio alizoshiriki Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya kimataifa ya michezo, CAS ilitupilia mbali rufaa ya Afrika Kusini iliyokuwa inapinga sheria mpya za shirikisho la riadha duniani IAAF, zinazotaka wakimbiaji wa kike wenye homoni zaidi zipunguzwe.

Semenya mwenyewe amesema "mimi ni mwanamke na mwanamichezo mahiri, IAAF haitanizuia jinsi nilivyo," alisema mwanariadha huyo.

Taarifa iliyotolewa Jumatano ya wiki hii inasema kuwa Semenya ataiomba mahakama ya Uswis itupilie mbali uamuzi wa Cas na kuongeza kuwa kiini cha rufaa yake ni haki ya msingi ya binadamu.

Wakili Dorothee Schramm ambaye ataongoza rufaa ya Semenya, amesema sheria za IAAF zinakiuka sheria za wazi kabisa za msingi za sera ya Uswis.

Kwa sheria za sasa, Casater Semenya na wanariadha wengine wa kike ambao homoni zao zimezidi kiwango, watahitajika kutumia dawa maalumu ili kuzipunguza waweze kushindana katika mbio za kuanzia mita 400.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.