Pata taarifa kuu
MICHEZO-SOKA

Klabu bingwa:Timu zitakazokutana robo fainali kujulikana leo

Droo ya hatua ya robo fainali kuwania taji la klabu bingwa na Shirikisho barani Afrika, inafanyika leo jijini Cairo nchini Misri. Mechi za robo fainali zitachezwa nyumbani na ugenini.

Uwanja wa soka wa Martyrs jijini Kinshasa moja ya viwanja vya mpira ambako zinachezwa mechi mbalimbali za kimataifa..
Uwanja wa soka wa Martyrs jijini Kinshasa moja ya viwanja vya mpira ambako zinachezwa mechi mbalimbali za kimataifa.. RFI/Habibou Bangré
Matangazo ya kibiashara

Katika kutafuta taji la klabu bingwa, klabu zitakazochuana ni pamoja na Wydad Casablanca kutoka Morocco, Esperance de Tunis kutoka Tunisia, TP Mazembe ya DRC, Al Ahly ya Misri.

Nyingine ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Horoya ya Guinea, CS Constaintine ya Algeria na Simba ya Tanzania.

Kwa upande wa taji la Shirikisho, klabu zinazosubiri droo hiyo ni pamoja na RS Berkane, Hassania Agadir zote za Morocco, CS Sfaxien na Etoile du Sahel kutoka Tunisia.

Zingine ni pamoja na Al-Hilal ya Sudan, Nkana kutoka Zambia, Zamalek ya Misri na Gor Mahia kutoka nchini Kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.