Pata taarifa kuu
KENYA-OLIMPIKI

Mahakama Kenya yaagiza kukamilishwa haraka uchunguzi dhidi ya viongozi wa kamati ya Olimpiki

Polisi nchini Kenya wamepewa majuma matatu kukamilisha uchunguzi kuhusu tuhuma kuwa wajumbe watatu wa kamati ya Olimpiki nchini humo wanaweza kuwa walichangia kukosekana kwa fungu la fedha, jezi na kuteseka kwa timu ya wanamichezo wa Kenya walioshiriki michezo ya Olimpiki ya Rio, Brazil iliyokamilika juma moja lililopita.

Makamu mwenyekiti wa kamti ya Olimpiki ya Kenya, Pius Ochieng na Francis Paul wakiwa mahakamni jijini Nairobi, 29 Agosti, 2016.
Makamu mwenyekiti wa kamti ya Olimpiki ya Kenya, Pius Ochieng na Francis Paul wakiwa mahakamni jijini Nairobi, 29 Agosti, 2016. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa msafara wa Kenya, Stephen Arap Soi, katibu mkuu wa kamati ya Olimpiki Francis Paul Kanyili na Meneja wa timu ya wanamichezo wa Kenya Pius Ochien, Jumatatu ya waiki hii waliachiwa kwa dhamana ya shilingi za kenya laki 2 kupisha kukamilika kwa uchunguzi, ambapo kesi yao itatajwa tena September 19 mwaka huu.

Kwa upande wake Nahodha wa timu ya wanamichezo wa Kenya walioshiriki Olimpiki ya Rio, Wesley Korir, ameeleza kufurahishwa na kinachofanywa hivi sasa na Serikali yake, na kuongeza kuwa ni lazima majibu yapatikane kujua kilichotokea kwa wanamichezo wa Kenya kushindwa kupata medali nyingi.

Toka kumalizika kwa michezo ya Olimpiki, kamati ya Olimpiki ya Kenya pamoja na wizara ya michezo, zimekosolewa kutokana na namna ambavyo wanamichezo wake walifanyiwa na kusihi maisha magumu na dhiki walipokuwa Brazil.

Wananchi wa Kenya pia walionesha gadhabu zao kupitia kwenye mitandao ya kijamii ambapo wameitaka Serikali kuwawajibisha viongozi waliohusika na kile kilichotajwa kuwa ni uzembe wa hali ya juu katika kutimiza majukumu yao.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ameagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina kubaini kilichotokea na kuwakumba karibu wanamichezo wote waliosafiri kwenda Rio, Brazil.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.