Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa Timu ya Taifa ya Uhispania

Imeshiriki mara 13, imewahi kutwaa taji hili mara 1, iko katika nafasi ya 1 kwenye viwango vya FIFA.Historia kwenye kombe la dunia la FIFA.Timu ya taifa ya Uhispania “La Seleccion” imewahi kulitwaa kombe hili la dunia la FIFA mara moja mwaka 2010 nchini Afrika Kusini. Katika mara zote ambazo timu ya taifa ya Uhispania imeshiriki kombe la dunia la FIFA kwa zaidi ya mara nane inaelezwa kuishia kwenye hatua ya robo fainali. 

Timu ya Taifa ya Uhispania
Timu ya Taifa ya Uhispania fifa.com
Matangazo ya kibiashara

Kundi ililopo.

Timu ya taifa ya Uhispania iko kwenye kundi B la michuano ya mwaka huu ikujumuishwa na timu ya taifa ya Uholanzi, Chile na Australia, hili ni kundi ambalo wachambuzi wanadai kuwa linatarajiwa kuwa na ushindani.

Wachezaji wa kuangaliwa.

Hakuna anayepinga kuwa kwasasa timu yenye wachezaji viungo bora zaidi duniani ni Uhispania, wachezaji kama Xavi, Andres Iniesta, Xabi Alonso wamekuwa ni kiungo muhimu kwenye timu hii. Wachezaji wengine ni pamoja na walinda mlango Iker Casillas wakati walinzi kama Sergio Ramos na Gerard Pique nao wakiongeza chachu kwenye timu. Wamo pia wachezaji kama Jordi Alba, David Villa, Fernando Torres, Pedro, Diego Costa, Alvaro Negredo na Cesc fabregas.

Benchi la Ufundi.

Timu ya taifa ya Uhispania inaongozwa na kocha mkongwe mwenye historia nzuri, Vicente del Bosque.

Mafanikio pekee kwenye fainali za kombe la dunia la FIFA.

Imefanikiwa kutwaa taji hili mwaka 2010 kwenye fainali zilizofanyika nchini Afrika Kusini, mwaka 1999 ilikuwa bingwa wa michuano ya vijana wa umri wa chini ya miaka 20 iliyofanyika nchini Nigeria na pia mwaka 1992 kama mabingwa wa Olympic iliyofanyika mjini Barcelona nchini Uhispania.

Waliowahi kuvuma.

Ni pamoja na Luis Suarez, Emilio Butragueno na Fernando Hierro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.