Pata taarifa kuu
IRAQ-USALAMA

Jeshi la Iraq ladhibiti uwanja wa ndege wa Mosul

Vikosi vya usalama vya Iraq vimeingia Alhamisi hii Februari 23, 2017 katika uwanja wa ndege wa Mosul, unaoshikiliwa na wapiganaji wa kundi la Islamic State na inasadikiwa kuwa wamechukua udhibiti kwa mujibu wa vyombo vya habari kadhaa nchini Syria.

Vikosi vya usalama vya Iraq, Februari 22, 2017 kusini mwa mji wa Mosul.
Vikosi vya usalama vya Iraq, Februari 22, 2017 kusini mwa mji wa Mosul. AHMAD AL-RUBAYE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la polisi la Iraq linaendelea na mashambulizi katika uwanja wa ndege unaopatikana kusini mwa Mosul. Kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali nchini Syria, kikosi hicho bado kinakabiliana na upinzani kutoka wapiganaji wa kundi la Islamic State. Kwa mujibu wa runinga ya taifa kikosi hicho kitapata ushindi na tayari kimechukua udhibiti wa uwanja huo.

Mashambulizi ya ardhini yanasaidiwa na ndege za muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani.

Kuurejesha kwenye himaya ya serikali uwanja wa ndege ni muhimu kwa serikali ya Iraq. Uwanja huu ni eneo muhimu, hata kama sehemu ndege zinaposhukia imeharibiwa. Pia ni moja ya sehemu ya kuingilia kuelekea eneo la magharibi mwa Mosul, ambapo bado linashikiliwa na wpiganaji wa IS.

Itakumbukwa kwamba, sehemu ya mashariki ya mji ilikombolewa mwezi uliopita. Lengo ni kuchukua udhibiti wa mji wa pili wa Iraq kwa ujumla. Katika mashambulizi yao, vikosi vya Iraq vinasaidiwa na muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani.

Mapigano ni makali. Kundi la Islamic State, ambalo bado lina wapiganaji 2,000 katika mji wa Mosul kwa mujibu wa shirika la ujasusi la Marekani, limeapa kupigana hadi dakika ya mwisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.