Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-MTANDAO-IS-UGAIDI-USALAMA

Saudi Arabia yakabiliwa na tishio la IS

Kwa mujibu wa Saudi Arabia, vita dhidi ya wanajihadi wa Daech lazima vipitie kwenye mitandao. Waziri wa mambo ya ndani wa Saudi Arabia, Mohammed bin Nayef anataka kuonesha kuwa hana hofu yoyote ya nchi yake kushmbuliwa na magaidi. Waziri huyo amechukua hatua za kukabiliana na ugaidi.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Saudi Arabia, Mohammed bin Nayef, Januari 23, mwaka 2015.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Saudi Arabia, Mohammed bin Nayef, Januari 23, mwaka 2015. REUTERS/Hamad I Mohammed/Files
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, mjini Riadh, Clarence Rodriguez, hatua hizi ziliyochukuliwa zinalenga hasa kuimarisha udhibiti juu ya mtandao na mitandao ya kijamii ya video zote za kunyongwa kwa mateka ziliyorushwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu.

Hatua hizi zinahusu pia masuala yote ya kisiasa, upinzani wa kidini na misimamo mikali ya upinzani au pia kurusha hewani taarifa ambayo ni kinyume na " maadili ya utawala kifalme". Inatosha kusema kuwa uwanja wa kujieleza umepunguzwa kwa asilimia kubwa.

Mitandao ya kijamii, Facebook, Twitter, Whatsapp, lakini pia simu za mkononi hatimaye zitafuatilia kwa karibu na kuchunguza kinachoendelea kwenye mitandao hiyo.

Ukiukaji wa masharti haya yataadhibiwa kwa miaka 3 jela na kupigwa bakora kwa raia wa Saudi Arabia. Kwa raia wa kigeni watachukuliwa hatua ya kufukuzwa kwenye aridhi ya nchi hiyo. Kuhusu hukumu ya kufungwa jela, inatofautiana kutoka miaka 3 hadi 30. Faini ni kutoka Yuro 200 hadi 600,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.