Pata taarifa kuu
RWANDA-CHINA-USHIRIKIANO-UCHUMI

Rais wa China azuru Rwanda, mikataba 15 kusainiwa

Rais wa China Xi Jinping na mwenyeji wake wa Rwanda Paul Kagame watakutana leo Jumatatu jijini Kigali, baada ya kuwasili Jumapili Julai 22. Xi Jinping anafanya ziara ya siku mbili nchini Rwanda, ikiwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kuzuru nchi hiyo.

Rais wa Rwanda Paul Kagame anatarajia kukutana na kutia saini mikataba 15 na rais wa China Xi Jinping ambaye yuko ziarani nchini Rwanda
Rais wa Rwanda Paul Kagame anatarajia kukutana na kutia saini mikataba 15 na rais wa China Xi Jinping ambaye yuko ziarani nchini Rwanda REUTERS/Ruben Sprich
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa waziri anayehusika na ushirikiano wa kimataifa Olivier Nduhungirehe amesema ziara ya kiongozi wa China Xi Jinping ni muhimu na imelenga kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili na kaongeza kuwa pamoja na raisi wa Rwanda Paul Kagame watasaini mikataba 15 kabla kiongozi huyo kutamatisha ziara yake.

Waziri Nduhungirehe pia amesema mataifa hayo mawili yatasaini pia makubaliano ya Jiolojia,upanuzi wa hospitali ya Masaka,ujenzi wa barabara na uwanja wa ndege wa Bugesera.

Xi Jinping amewasili nchini Rwanda baada ya kutamatisha ziara yake huko Senegal ambako pia amesaini mikataba 15 ya kibiashara, naye atatamatisha ziara yake nchini Rwanda leo Jumatatu na ataelekea nchini Afrika kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.