Pata taarifa kuu
UGANDA-MUSEVENI-USALAMA

Rais Museveni amfuta kazi Mkuu wa Jeshi la Polisi na Waziri wa Usalama

Rais wa Uganda amemfuta kazi Waziri wa usalama Henry Tumukunde na Mkuu wa Jeshi la Polisi Janerali Kale Kayihura, ambaye amekuwa akiongoza kikosi cha polisi muda mrefu.

Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uganda  Kale Kayihura
Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uganda Kale Kayihura Gaël Grilhot/RFI
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya Museveni imekuja wakati huu, baada ya kuonekana tofauti za kiutendaji kati ya Kaihura na Tumukunde lakini kufutwa kwao kazi, hakukutarajiwa.

Uamuzi huo ulitangazwa kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Kyaihura kabla ya kufutwa kazi, alionekana kuwa karibu sana na rais Museveni ambaye hivi karibuni amekuwa akidai kuwa jeshi la Polisi limeingiliwa na watu ambao sio waaminifu, aliowaita wahalfu.

Wachambuzi wa siasa na usalama nchini Uganda wamekuwa wakisema kuwa, rais Museveni ameonekana kutowaamini viongozi hao wa usalama na ameamua kuachana nao.

Kayihura amemshukuru rais Museveni kwa  kumteua katika nafasi hiyo na kukiri kuwa nyakati, alimwangusha rais Museveni katika utendaji kazi wake.

'Ninamshukuru rais Museveni kwa kuniteua katika wadhifa huu, naahidi kuwa nitaendelea kufanya bidii kwa muda wangu unaosalia katika maisha yangu,” alisema Kayihura.

Kabla ya kuteuliwa kwake mwaka 2005,  Kayihura ambaye pia ni Wakili na aliyepata mafunzo ya kijeshi nchini China, alihudumu katika nyadhifa mbalimbali katika jeshi la UPDF.

Akiwa jeshini, aliwahi kuongoza jeshi la Uganda kupambana na waasi katika mkoa wa Ituri nchini DRC.

Kayihura, atakumbukwa kuwa mshirika wa karibu wa rais Museveni aliyetumia nguvu dhidi ya kiongozi wa upinzani nchini humo Kizza Besigye.

Nafasi ya Kayihura imechukuluwa na Okoth Ochola ambaye alikuwa naibu wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.