Pata taarifa kuu
KENYA-HAKI-UCHAGUZI

Baadhi ya wabunge wa Jubilee wataka Jaji mkuu afutwe kazi

Saa chache baada ya baadhi ya wabunge wa chama cha Jubilee kupeleka malalamiko kwa tume ya kuwaajiri majaji wakitaka kuondolewa kazini kwa jaji mkuu David Maraga, katibu mkuu wa chama hicho Rafael Tuju amejitokeza na kukanusha kuwa ni msimamo wa chama chao.

David Maraga (katikati), Jaji Mkuu wa mahakama ya Juu ya Kenya.
David Maraga (katikati), Jaji Mkuu wa mahakama ya Juu ya Kenya. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Mapema leo asubuhi mbunge wa Nyeri Njiri Wambungu aliwasilisha kesi kwa tume ya majaji akitaka jaji Maraga aondolewe kazini kwa kile alichodai ni kushindwa kumtambua Uhuru Kenyatta kama rais halali wa Kenya na kubatilisha uchaguzi wa mwezi uliopita.

Mbunge huyo wa Nyeri, Njiri Wambugu amewasilisha ombi lake mbele ya tume ya huduma za majaji akidai kwamba jaji Maraga alihusika katika kufanya makosa.

Akihutubia vyombo vya habari, Bw, Wambungu anadai kwamba Jaji David Maraga 'aliwashinikiza' wenzake kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa rais Uhuu Kenyatta wakati alipotoa uamuzi wa kihistoria mnamo tarehe 1 Septemba.

Haya yanajiri wakati waangalizi wa Uchaguzi wa urais nchini Kenya kutoka Umoja wa Ulaya, wameitaka Tume ya Uchaguzi kuhakikisha kuwa inafanya mabadiliko muhmu kuelekea Uchaguzi wa urais mwezi ujao.

Waangalizi hao wanaitaka Tume ya Uchaguzi kuja na mfumo utakaokuwa wazi wa kuhesabu na kujumuisha matokeo ya urais.

Waangalizi hao wamekutana na Tume ya Uchaguzi jijini Nairobi kujadiliana kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa mwezi ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.