Pata taarifa kuu
KENYA-KESI-UCHAGUZI

IEBC yasema mitambo yake ya matokeo ipo Ulaya

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya inasema mitambo yake yenye matokeo halisi ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mapema mwezi huu, ipo barani Ulaya.

Wafula Chebukati, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya
Wafula Chebukati, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBCKenya
Matangazo ya kibiashara

Kupitia kwa Wakili wake Paul Muite, IEBC imeambia Mahakama Kuu jijini Nairobi kuwa haijakataa kuwapa nafasi Mawakala wa upinzani kuangalia mitambo hiyo.

Hatua hii imekuja baada ya Mawakili wa Upinzani wanaomwakilisha Raila Odinga, anayepinga ushindi wa rais Uhuru Kenyatta kuiambia Mahakama kuwa, Tume ya Uchaguzi ilikuwa imekataa kutii agizo lake.

Siku ya Jumatatu, Mahakama iliruhusu pande zote kuangalia na kupitia mitambo ya Tume ya Uchaguzi na ripoti kuwasilishwa Mahakamani kufikia saa 11 jioni.

Jaji Mkuu David Maraga, ameagiza kuwa uamuzi wa Mahakama hiyo uheshimiwe na ripoti kuwasilishwa hivi leo.

Siku ya Jumanne, upande wa utetezi umekuwa ukitoa ushahidi kupinga utetezi wa kiongozi wa upinzani NASA, Raila Odinga anayetaka matokeo yaliyompa ushindi kutupiliwa mbali.

Uamuzi wa mwisho unatarajiwa kutolewa siku ya Ijumaa huku kesi hiyo ikitarajiwa kumalizika hivi leo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.