Pata taarifa kuu
TANZANIA

Rais Magufuli amfuta kazi Waziri wa Nishati na Madini

Rais wa Tanzania John Magufuli amemfuta kazi Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo .

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli
Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli Screenshot/Azama TV
Matangazo ya kibiashara

Magufuli amefanya uamuzi huo saa chache baada ya  kupokea ripoti kuhusu mchanga wa madini, uliozuliwa kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

Imebainika kuwa kiwango cha madini ndani ya mchanga huo uliokuwa ndani ya makontena zaidi ya 200 yaliyochunguzwa  yalikuwa na dhahabu yenye thamani ya zaidi ya shilingi Trilioni moja za nchi hiyo.

Serikali ya Tanzania imekuwa ikisema inapata hasara katika usafirishaji wa mchanga wa madini katika miaka iliyopita.

Rais Magufuli amesema Waziri Muhongo ameshindwa  kusimamia Wizara yake kama ilivyotarajiwa hasa kuhusu maswala ya madini.

“Profesa Muhongo nampenda sana lakini pia ni rafiki yangu, lakini katika hili, ajithathmini na aachie madaraka,” alisema rais Magufuli.

Wakati uo huo, rais Magufuli amevunja Bodi ya wakala wa ukaguzi wa madini nchini humo na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.