Pata taarifa kuu

Raia wa Uingereza ashinda mbio za Tour de France

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amempongeza mkimbiza baiskeli wa Uingereza Bradley Wiggins kwa mafanikio aliyoyapata katika mashindano ya mbio za baiskeli.

REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Cameron amesema kuwa ushindi huo ni heshima kubwa kwa Uingereza.

Mkimbiza baiskeli wa Uingereza Bradley Wiggins amekuwa Mwingereza wa kwanza kushinda mashindano ya baiskeli ya Tour de France.

Wiggins kijana wa miaka 32 alimalizia mashindano hayo katika mitaa ya jiji la Paris kwa ushindi mdogo wa dakika tatu na sekunde 21 na kuandika historia katika mashindano hayo.

Katika hatua nyingine mkimbiza baiskeli mwenzake kutoka timu ya Sky, ya Uingereza Chris Froome yeye alifanikiwa kushika nafasi ya pili na huku Vincenzo Nibali wa Italia akinyakua nafasi ya tatu.

Hiyo ilikua ni nafasi maalum kwa Wiggins ambaye alipita katika mitaa ya Paris na kupata ushindi huo wa kushangaza huku akishangiliwa na mashabiki waliokuwa wakifuatilia mashindano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.