Pata taarifa kuu
VIETNAM-UINGEREZA-USALAMA-HAKI

Miili iliopatikana katika lori karibu na London yarudisha nchini Vietnam

Miili 16 kati ya 39 ya raia wa Vietinam iliopatikana mwezi uliopita katika kasha la gari ya mizigo katika mji wa Essex karibu na London imerudishwa nchini Vietnam, mwakilishi wa Vietnam na vyombo vya habari nchini vimeripoti leo Jumatano.

Polisi ikiondoa miili 39 iliyopatikana katika kasha la gari ya mizigo, Grays, katika mji wa Essex, Uingereza Oktober 23, 2019.
Polisi ikiondoa miili 39 iliyopatikana katika kasha la gari ya mizigo, Grays, katika mji wa Essex, Uingereza Oktober 23, 2019. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Miili ya wanaume 31 na wanawake wanane ilipatikana usiku wa tarehe 22 kuamkia 23 Oktoba baada ya gari ya mizigo waliokuwemo kuwasili katika eneo la bandari la Purfleet, karibu na mji wa London. Gari hilo lililokuwa na namba za usajili za Bulgaria liliingia nchini Uinreza likitokea Zeebrugge, nchini Ubelgiji.

Dereva wa lori hilo, raia wa Ireland ya Kaskazini, mwenye umri wa miaka 25, ameshtakiwa kwa makosa 39 ya mauaji, biashara ya binadamu na utakatishaji pesa.

Watu wanane walikamatwa mwezi huu nchini Vietnam, na kupelekea idadi ya watu waliokamatwa nchi humo kufikia 10.

Kulingana na tovuti ya habari ya VnExpress, miili ya watu hao iliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Hanoi Jumatano hii asubuhi. Maiti zingine zitarejeshwa nchini Vietnam baadaye.

Familia za wahanga zitalazimika kulipa gharama za usafiri wa miili ya ndugu zao, kwa mujibu shirika la Habari la Reuters ikinukuu taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Vietnam.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.