Pata taarifa kuu
URUSI

Rais Putin amfuta kazi mkuu wa Polisi aliyemkamata mwanahabri

Siku chache baada ya mwandishi wa habari za uchunguzi wa Urusi Ivan Golunov kuachiwa baada ya maandamano, rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza kumfuta kazi afisa wa juu wa polisi mjini Moscow.

Rais wa Urusi, Vladmir Putin.
Rais wa Urusi, Vladmir Putin. 路透社。
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya ndani wa Urusi alitoa wito wa kufutwa kazi kwa mkuu wa Polisi katika eneo ambalo mwanahabari huyo alikamatwa.

Mbali na afisa huyo wa polisi, rais Putin pia amemfuta kazi mkuu wa kitengo cha udhibiti wa dawa za kulevya.

Mwandishi wa habari Golunov aliachiwa huru juma hili baada ya maandamano ya wananchi na wanahabari wengine wakipinga namna alivyokamatwa.

Golunov alikamatwa akiwa anaelekea kukutana na mtoa taarifa wake ambapo polisi ilidai alikuwa anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Taarifa zinasema hata picha zilizotumiwa na polisi kuonesha kukamatwa kwa vifaa vya kutengenezea dawa hizo hazikuchukuliwa kutoka katika makazi yake.

Mamia ya watu walikamatwa wakati wa maandamano ya kushiniliza Golunov kuachiwa wengi wakiwa na mabango ya kuishutumu polisi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.