Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Christchurch: Mtuhumiwa akabiliwa na mashitaka 50 ya mauaji

media Brenton Harrison Tarrant, raia wa Australia mwenye umri wa miaka 28, ambaye alitambuliwa kama mtu mwenye msimamo mkali wa ubaguzi wa rangi, anatuhumiwa kuua watu 50 na kujeruhiwa wengine kadhaa, Machi 15, wakati wa sala ya Ijumaa katika misikiti miwili. REUTERS/Mark Mitchell

Mtuhumiwa wa mauaji katika Misikiti miwili ya Christchurch, nchini New Zealand anakabiliwa na mashitaka 50 ya mauaji na mashitaka thelathini na tisa ya jaribio la mauaji, polisi ya nchi hiyo imesema.

Mashtaka mengine bado yanajadiliwa, polisi imesema katika taarifa yake.

Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern, ameliita shambulio hilo kama "kitendo cha kigaidi." New Zealand haijawahi kukumbwa na tukio baya la mauaji ya watu wengi kama hilo.

Brenton Harrison Tarrant, raia wa Australia mwenye umri wa miaka 28, ambaye alitambuliwa kama mtu mwenye msimamo mkali wa ubaguzi wa rangi, anatuhumiwa kuua watu 50 na kujeruhiwa wengine kadhaa mnamo Machi 15, wakati wa sala kuu ya Ijumaa katika misikiti miwili huko Christchurch.

Tarrant, ambaye alishtakiwa kwa mauaji wakati aliposikilizwa kwa mara ya kwanza katika mahakama siku moja baada ya shambulio, anatarajiwa kufikishwa mbele ya mahakama kuu Ijumaa wiki hii.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana