Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-ITALIA-SIASA

Mwakilishi wa Korea ya Kaskazini Italia aomba hifadhi ya ukimbizi

Gazeti kuu la kila siku la Korea Kusini la JoongAng Ilbo,  likinukuu vyanzo kadhaa vya kidiplomasia mjini Seoul limesema balozi wa Korea Kaskazini nchini Italia, ametoroka na familia yake na kuomba hifadhi katika nchi ya magharibi.

Kama taarifa hiyo itathibitishwa, Jo Sung-gil atakuwa afisa mwengine mwandamizi kutoroka na itakuwa ni pigo kubwa kwa serikali ya Pyongyang.
Kama taarifa hiyo itathibitishwa, Jo Sung-gil atakuwa afisa mwengine mwandamizi kutoroka na itakuwa ni pigo kubwa kwa serikali ya Pyongyang. LILLIAN SUWANRUMPHA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jo Sung-gil, 48, aliongoza ubalozi wa Korea Kaskazini mjini Roma tangu mwezi Oktoba 2017, wakati mamlaka nchini Italia ilimfukuza balozi wa nchi hiyokufuatia jaribio la sita kinyuklia la Korea Kaskazini. Kama taarifa hiyo itathibitishwa, Jo Sung-gil atakuwa afisa mwengine mwandamizi kutoroka na itakuwa ni pigo kubwa kwa serikali ya Pyongyang.

Balozi huyo wa Korea Kaskazini aliomba hifadhi ya ukimbizi kwa serikali ya Italia mapema mwezi Desemba, Gazeti la kila siku la JoongAng limebaini mapema leo asubuhi. Gazeti hilo limeongeza kuwa baada ya Italia kusita, hatimaye imekubali kumpa hifadhi ya ukimbi balozi huyo.

Sababu ya kutoroka kwake hazijajulikana. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Korewa Kusini, Jo Sung-alipewa agizo la kurejea nyumbani (Pyongyang). Lakini alipendelea kutoroka na mke wake na watoto. Balozi huo bila shaka alikuwa na cheo cha juu katika utawala wa Pyongyang. Ni nadra serikali ya Pyongyang kuruhusu wanadiplomasia wake kuongozana na familia zao, hatua ya kuzuia kutoroka.

Serikali ya Korea Kusini, ambayo inatafuta kuboresha uhusiano wake na jirani yake Korea Kaskazini, bado haijathibitisha taarifa hiyo. Thae Yong-ho, naibu balozi wa Korea Kaskazini mjini London, ni afisa wa ngazi ya juu nchini humo kutoroka na kuomba ukimbizi nchini Korea Kusini mnamo mwaka 2016. Thae Yong-ho yuko mafichoni tangu wakati huo, chini ya ulinzi wa idara ya ujasusi, kwa hofu ya kufanyiwa maovu na serikali ya Pyongyang.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.