Pata taarifa kuu
MALAYSIA-KOREA KASKAZINI-USHIRIKIANO

Wanawake wawili wahusishwa na kifo cha Kim Jong Nam

Wanawake wawili waliokamatwa kwa madai ya kuhusika na kifo cha ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini, watafunguliwa mashtaka ya kuhusika na kifo cha Kim Jong-nam nchini Malaysia.

Maandamano nje ya ubalozi wa Korea Kaskazini kupinga dhidi ya mauaji ya ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-nam, 13 Februari.
Maandamano nje ya ubalozi wa Korea Kaskazini kupinga dhidi ya mauaji ya ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-nam, 13 Februari. REUTERS/Athit Perawongmetha
Matangazo ya kibiashara

Jaji mkuu wa Mahakama ya nchini Malaysia, amesema wanawake hao wawili mmoja akijulikana kwa jina la Siti Aisyah, mwenye umri wa 25, kutoka Indonesia na mwingine Doan Thi Huong, mwenye umri wa 28, kutoka Vietnam wanadaiwa kumuua ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Nam watajibu mashtaka dhidi yao kwa kutumia sumu kali kuuwa katika uwanja wa ndege mjini Kuala Lumpar.

Wanawake hao ni miongoni mwa watu kumi ambao wanashukiwa na Malaysia kwamba huenda walihusika na mauaji hayo.

Vyanzo vya kisheria nchini Malaysia vimesema wanawake hao watashtakiwa chini ya sheria ya nchi na iwapo watapatikana na hatia watanyongwa.

Malaysia inasema, Bwana Kim aliyekuwa mkosoaji wa nduguye, aliuwawa kwa kutumia sumu kali ambayo imepigwa marufuku na Umoja wa mataifa.

Washukiwa hao wawili wanadaiwa kumpaka usoni kemikali hiyo ya sumu katika uwanja wa ndege wa Malaysia mapema mwezi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.