Pata taarifa kuu
HUAWEI-MAREKANI-HAKI

Huawei yafungulia mashitaka Marekani

Kampuni ya simu ya Huawei kutoka nchini China imeifungulia kesi serikali ya Marekani, baada ya kuzuia mashirika ya umma kutumia vifaa vya kampuni yake.

Marekani yazuia mashirika ya umma kutumia vifaa vya kampuni kubwa ya simu Huawei.
Marekani yazuia mashirika ya umma kutumia vifaa vya kampuni kubwa ya simu Huawei. REUTERS/Dado Ruvic
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Marekani imezuia mashirika yake kutumia vifaa vya kampuni hiyo kama simu na vingine vya eletroniki kwa madai kuwa, ni hatari kwa usalama wake.

Mwenyekiti wa kampuni ya Huawei Guo Ping, amewashtumu wabunge na serikali ya Marekani kwa kushindwa kuthibitisha madai hayo, na uamuzi wa kwenda Marekani umekuwa wa mwisho, ili kupata suluhu.

Kesi hiyo imewasilishwa katika Mahakama mjini Texas na katika utetezi wake, inatarajiwa kueleza kuwa haina ushirilkiano wowote na serikali ya China kama Marekani inavyoadai.

Mbali na Marekani, Australia na New Zealand, zimeweka vikwazo kwa kampuni za nchi zao kutumia vifaa vya mawasiliano na teknolojia kutoka Huawei.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.