Pata taarifa kuu
UN-MAREKANI-URUSI-SYRIA

Haley: Ni aibu kwa UN kushindwa kuzuia mauaji Syria

Balozi wa Marekani kwenye umoja wa Mataifa Nikki Haley Jumatano hii amelikosoa vikali baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa kushindwa kuzuia mashambulizi kwenye mji wa Ghouta mashariki nchini Syria.

Balozi wa Marekani kwenye umoja wa Mataifa Nikki Haley.
Balozi wa Marekani kwenye umoja wa Mataifa Nikki Haley. REUTERS/Eduardo Munoz
Matangazo ya kibiashara

Kwenye hotuba yake kwa baraza la usalama, Haley amesema ni 'aibu' kwa baraza hilo kushindwa kusimamia azimio la usitishaji wa mapigano kwa muda wa siku 30 nchini Syria.

Nchi ya Urusi hata hivyo ilijibu mapigo kwa kudai kuwa ndio taifa pekee kwenye umoja wa Mataifa ambalo linasimamia na kuhakikisha makubaliano ya usitishaji wa mapigano nchini Syria yanaheshimiwa.

"Hii inabidi iwe siku ya aibu kwa kila mwanachama wa baraza hili," alisema Helry.

Haley amesema zaidi ya watu 1600 wameuawa huku baraza hilo likitazama, tangu baraza la usalama litangaze azimio la usitishaji wa mapigano kwenye mji wa Ghouta Februari 24 mwaka huu, kumekuwa na mazungumzo ya kina kati ya Urusi na mshirika wake rais Bashar al-Asad katika kusitisha mapigano kwenye mji huo.

Maelfu ya raia wa Syria wameendelea kupakiwa kwenye mabasi kutoka kwenye mji wa Ghouta siku ya Jumanne katika kile nchi za maghribi zinaona ni njama ya Urusi na utawala wa Damascus kuendelea kushambulia mji huo.

Balozi wa Urusi kwenye umoja wa Mataifa Vassily Nebenzia amesema kuondoka kwa maelfu ya wapiganaji na raia ni uamuzi wao binfasi hawakulazimishwa na kwamba utawala wa Moscow umekuwa ukitoa msaada wa chakula na mahitaji mengine kwa raia.

Nchi ya Ufaransa yenyewe imeeleza kuguswa na hatma ya watu elfu 55 wanaohifadhiwa kwenye makambi maalumu yanayosimamiwa na Serikali ya Syria mashariki mwa mji wa Ghouta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.