Pata taarifa kuu
SYRIA

Syria: Waasi wa Ghouta wakubali kusitisha mapigano na kuondoka

Makundi ya waasi mashariki mwa mji wa Ghouta nchini Syria yametangaza usitishaji wa mapigano kuanzia usiku wa kuamkia leo baada ya wapiganaji na familia zao kuondoka kwenye mji huo chini ya makubaliano yaliyosimamiwa na Urusi yakiwa ni ya kwanza tangu kuanza kutekelezwa kwa mashambulizi kwenye mji huo.

Baadhi ya wapiganaji waasi na familia zao wakiondoka kwenye mji wa Harasta mjini Ghouta, Syria. 22 Machi 2018.
Baadhi ya wapiganaji waasi na familia zao wakiondoka kwenye mji wa Harasta mjini Ghouta, Syria. 22 Machi 2018. REUTERS/Omar Sanadiki
Matangazo ya kibiashara

Watu walioondoka kwenye mji huo walipandishwa kwenye mabasi kuelekea kaskazini mwa mji wa Idlib baada ya saa kadhaa za kusubiri kabla ya kuruhusiwa kupita kwenye maeneo yanayokaliwa na vikosi vya Serikali.

Kwenye mji wa Idlib ambako ni mji wa mwisho ambao vikosi vya Serikali havina umiliki, shambulio la anga kwenye soko moja liliua watu 28m imesema taarifa ya shirika moja la kutetea haki za binadamu.

Makubaliano ya kuruhusu waasi kuondoka kwenye mji huo yalitangaza siku ya Jumatano, makubaliano yaliyosimamiwa na Urusi na utawala wa Damascus ambapo sasa maeneo matatu yaliyokuwa yanakaliwa na waasi yatakuwa matupu.

Hatua ya kundi hili itayafanya makundi mengine mawili yanayoshikilia sehemu ya mji huo kubaki peke yao kwenye mji wa Ghouta na kuwashinikiza na wao kukubali kuweka silaha chini na kuondoka.

Hatua hii imekuja baada ya msemaji wa kundi la Faylaq al-Rahman la kusini mwa mji wa Ghouta kutangaza kufikia makubalian ya kusitisha mapigano chini ya makubaliano na umoja wa Mataifa.

Makubaliano haya ya usitishaji wa mapigano kutaruhusu mzunguko wa mwisho wa mazungumzo kati ya waasi na Urusi, taarifa hiyo iliongeza.

Jumla ya watu 1580 wakiwemo wapiganaji 413 waliondoka kwenye mji wa Ghouta wa Harasta wakiwa kwenye mabasi 30, kimesema kituo cha televisheni cha SANA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.