Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-USAFIRI

Agizo kuhusu visa nchini Marekani: Donald Trump aikosoa mahakama

Baada ya kusikilizwa kwa njia ya simu Jumanne, Februari 7, kinachosubiriwa sasa ni uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ya Marekani kuhusu agizo la visa la Donald Trump.

Donald Trump (hapa likua Februari 3) akisaini agizo la kupiga marufuku raia kutoka mataifa saba ya Kiislamu kwa muda wa miezi mitatu.
Donald Trump (hapa likua Februari 3) akisaini agizo la kupiga marufuku raia kutoka mataifa saba ya Kiislamu kwa muda wa miezi mitatu. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani amekosoa vikali vyombo vya sheria vya Marekani kuingizwa katika mambo ya kisiasa. Msimamo ambao tayari umeanza hali ya sintofahamu kwa wabunge kutoka chama cha Republican na wale kutoka chama cha Democratic.

Baada ya kuhojiwa maswali kutoka pande zote, majaji wa San Francisco walikataa kubadili msimamo wao kwa shinikizo na wanajaribu kufikiri kuchukua uamuzi mkali. Wametangaza katika taarifa yao kuwa pande zinazohusika zitafahamishwa kabla ya kutangazwa kwa uamuzi wao. Licha ya shinikizo kutoka vyombo vya habari, na Ikulu ya White House, rais wa Marekani ameonyesha dharau yake kwa mahakama baada ya kesi hiyo kusikilizwa. "Nilisikiliza yote haya jioni ya Jumatatu kwenye televisheni, ilikuwa ni aibu, aibu .... Tishio la kigaidi lipo kinyume na jinsi watu wanavyoelewa, " amesema Donald Trump.

Vyombo vya habari vya Marekani vinaaelewa kuwa wanasheria kutoka Wizara ya Sheria na Ikulu ya White House wamekataa tamaa baada ya kauli hii ya rais. Mwakili wa chama cha Republican Kizinger, anaeunga mkono agizo kuhusu visa, anakubaliana kuwa madai hayo ya rais hayana maana yoyote: "Ni lazima kuheshimu uamuzi wa majaji. Na kama unakubaliana au la na uamuzi huo, nadhani ni mbinu mbaya kushambulia majaji. "

Jenerali Kelly, kutoka Wizara ya Usalama wa Taifa, anatambua kwa upande wake kwamba utekelezaji wa agizo la rais Donal Trump uliendeshwa haraka sana. "Ni kosa langu, almesema mbele ya Bunge la Congress, ningelishelewesha utekelezaji wake. Hivyo tungelizuia hali ya sintofahamu iliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita. "

Donald Trump ameendelea kukosolewa kutoka mataifa mbalimbali kutokana na msimamo wake, hasa ule wa kupinga raia wa kigeni kuingia au kuishi nchii Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.