Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-USAFIRI

Wanasheria wa utawala wa Trump wapata usumbufu kwa kutetea agizo lake

Agizo la rais wa Marekani Donald Trump kuhusu visa lilikuwa Jumanne, Februari 7 mbele ya Mahakama ya Rufaa ya California. Ikulu ya White House inajaribu kutetea agizo hilo linalopiga marufuku raia kutoka mataifa saba ya Kiislamu kuingia nchini Marekani. Agizo ambalo mahakama ya shirikisho katika jimbo la Washington ilizuia.

Mahakama ya rufaa ya San Francisco yanatathmini agizo dhidi ya wahamiaji lililotolewa na Donald Trump.
Mahakama ya rufaa ya San Francisco yanatathmini agizo dhidi ya wahamiaji lililotolewa na Donald Trump. REUTERS/Noah Berger
Matangazo ya kibiashara

Majaji watatu walisikia kwa njia ya simu, hoja za pande zote mbili. Kesi hiyo ilirushwa hewani kwenye mitandao ya kijamii.

Pamoja Washington mwandishi wetu, Anne-Marie Capomaccio

Kama Donald Trump alikuwa mbele ya televisheni yake, aliona kama watumiaji wengine wa Intaneti jinssi gani wakili aliyekuwa akitetea agizo lake dhidi ya wahamiaji alivyosumbuka kwa kutetea agizo hilo. Katika utetezi wake wakili huyo alisema kuwa rais wa Marekani anahisi kwamba bado kuna hatari ya kuwepo kwa mashambulizi ya kigaidi katika ardhi ya Marekani. Majaji watatu walionyesha msimamo wao bila kuegemea. "Jaji Clifton alisema: Nakuelewa na hiyo ni dhana, lakini hoja hiyo haina msingi! Je, kuna sababu yoyote ya msingi, inayokufanya kufikiria kutokea kwa hali hiyo? "

Jaji mwengine aliuliza: Ni mashambulizi mangapi yaliyotekelezwa na watu kutoka nchi hizo saba zilizotajwa? Je, una ushahidi ambao mnatuficha? Mwanasheria wa Ikulu ya White House alipewa nafasi ya kujitetea kwa muda wa dakika thelathini.

Wakili wa jimbo la Washington hatimaye alitetea uamuzi wa kuzuia utekelezaji wa amri hiyo ya rais.

Hayo yakijri uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ya San Francisco unatarajiwa kutolewa kabla ya mwisho wa wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.