Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Kenya yazindua mradi tata wa ujenzi wa reli ya kisasa

media Mradi huu mpya wa reli ya kisasa unaounganisha Nairobi na Susua umezua utata nchini Kenya, haswa kwa sababu ya gharama yake. © SIMON MAINA / AFP

Mradi wa reli ya kisasa maarufu SGR utakaounganisha uwanja wa Kimataifa wa Jommo Kenyatta hadi jijini Nairobi umezinduliwa na rais Uhuru Kenyatta. Ujenzi wa reli hii ya kisasa ya standard GAUGE itagharimu dola za kimarekani bilioni 1.5.

Mradi huu ni matokeo ya ziara ya rais Kenyatta mwezi septemba mwaka uliopita katika taifa la China,kwenye kongamano lililowaleta pamoja viongozi wa Afrika pamoja na wawekezaji.

Mradi huu utatekelezwa na kampuni ya ujenzi wa barabara na madaraja ya China, kwa ushirikiano na serikali ya Kenya na mashirika ya kibinafsi.

Mradi huu mpya wa reli ya kisasa unaounganisha Nairobi na Susua umezua utata nchini Kenya, haswa kwa sababu ya gharama yake.

Tofauti na uzindizi wa reli ya kutoka Mombasa hadi Nairobi, ilivyozinduliwa kwa mbwembwe mwaka 2017, uzinduzi wa reli hii mpya haujapewa umuhimu mkubwa.

Wachambuzi wanasema Serikali inakabiliwa na wakati mgumu kuelezea faida za kiuchumi za mradi huo kwa sababu baadhi ya vituo havina shughuli nyingi katika mkoa wa bonde la ufa.

Rais Uhuru Kenyatta amewalauamu baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wengine ambao wameendelea kukosoa mradi huo.

"Wengine wanasema ooh! hii reli inaenda wapi? hakuna kitu kibaya kama ujinga wa mtu ambaye fikra zake ni namna hii. Sasa sisi tukisema tunajenga hii kusaidia wananchi tatizo liko wapi?", alisema Kenyatta. 

Rais Kenyatata ameongeza kuwa reli hiyo itapunguza msongamano mkubwa wa magari

Hata hivyo wataalam wanasema kuwa mradi huu ni ghali mno ikilinganishwa na gharama inayostihili kuchukuliwa huku ushirikiano kati ya China na Afrika ukiendelea kupanuka.

Barabara hiyo itakuwa na urefu wa kilomita 17. Badala ya kuchukua saa nyingi kufika uwanja wa kimataifa, barabara hiyo itakapokamilika mtumiaji atatumia dakika 10 au 15 kutoka katikakati ya jiji.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana