Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO

Wabunge wa Uingereza wafutilia mbali mpango wa kujitoa katika EU

Wabunge wa Uingereza wamefutilia mbali mkataba wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya uliofikiwa kati ya serikali ya Theresa May na Umoja wa Ulaya. Dakika chache kabla ya kura hiyo kupigwa, Waziri Mkuu Theresa May amewaomba wabunge "kuheshimu (...) matokeo ya kura ya maoni".

Wabunge wa Uingereza wakipiga kura dhidi ya mkataba wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya, London, Januari 15, 2019.
Wabunge wa Uingereza wakipiga kura dhidi ya mkataba wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya, London, Januari 15, 2019. Reuters TV via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kukataliwa kwa mpango huo ni pigo kubwa kwa Theresa May na serikali yake. Wabunge hawakujali ahadi iliyotolewa na Theresa May ya kufanya kazi kwa karibu zaidi na bunge wala wito kwa viongozi waliochaguliwa kutosaliti uamuzi wa wawanchi wa Uingereza kupiga kura ya kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Wabunge wamekataa mpango wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya kwa kura 432 dhidi ya 202.

Hili ni pigo kubwa kwa serikali ya Uingereza katika historia ya nchi hiyo, amesema mwandishi wetu mjini London, Muriel Delcroix.

Ingawa sio mshangao, kushindwa kwa Theresa May kunaongeza wasiwasi unaoendelea kuikumba Uingereza kwa sasa. Pia inatoa tumaini kwa wengine.

Uamuzi wa wabunge umekaribishwa na wafuasi wanaotaka kupigwa kura mpya ya maoni.

Hivi karibuni wanasiasa mbalimbali walitoa wito wa kufanyika kwa kura mpya ya maoni ili kuondokana na mgogoro wa kisiasa unaoendelea.

Hata hivyo serikali ya Theresa May ilifutilia mbali hoja hiyo, ikisema itazidisha mgawanyiko na kukiuka uamuzi wa wananchi wa Uingereza ambao walipiga kura Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya mnamo mwaka 2016.

Muda wa mwisho Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya utakamilika Machi 29, 2019 siku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.