Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Joto la kisiasa laendelea Uingereza

Kiongozi wa upinzani nchini Uingereza Jeremy Corbyn, amewasilisha mswada wa kukosa imani na Waziri Mkuu Theresa May. Miezi miwili iliyopita Jeremy Corbyn alisema chama chake cha Labour kitapiga kura kupinga mpango wa Waziri Mkuu Theresa May kuhusu nchi hiyo kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya.

kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour, Jeremy Corbyn, wa siasa za mrengo wa kushoto.
kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour, Jeremy Corbyn, wa siasa za mrengo wa kushoto. REUTERS/Peter Nicholls
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja, baada ya Waziri Mkuu May kuahirisha upija kura wa kuunga au kukata mkataba wa nchi hiyo kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya, hadi tarehe 14 mwezi Januari.

Corbyn, amesema haikubaliki kwa Waziri Mkuu kuchelewesha upigaji kura na kumlaumu kwa kuiweka nchi hiyo kwenye mzozo.

Hata hivyo, ripoti zinasema kuwa serikali haitatenga muda kwa muswada huo kujadiliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.