Pata taarifa kuu
UKRAINE-VITA-USALAMA-SIASA

Ukraine: zaidi ya watu 9,000 wameuawa tangu kuanza kwa machafuko

Zaidi ya watu 9000 wameuawa tangu kuanza kwa machafuko mashariki mwa Ukraine, kwa kipindi cha miezi ishirini sasa. Kamishna mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ametoa ripoti yake ya miezi mitatu kuhusu suala la mauaji yanayoendelea kushuhudiwa nchini Ukraine.

REUTERS/Alexander Ermochenko
Matangazo ya kibiashara

Hata kama machafuko yamepungua, shirika la Umoja wa Mataifa lina wasiwasi kuhusu hali ngumu ya kibinadamu na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Mauaji, mateso, kusumbuliwa, kizuiliwa kinyume cha sheria, kazi ya kulazimishwa ... kuna vitendo viovu ambavyo vimekua vikiwekwa wazi na wachunguzi wa Umoja wa Mataifa katika maeneo yaliojitnga ya Donetsk na Lugansk. Kukosekana kwa utawala wa sheria na mamlaka halali imewanfanya raia kutopata ulinzi wa kutosha na kutotendewa haki na vyombo vya sheria.

Maisha magumu kwa raia

Mbali na visa hivyo, hali ya maisha ya kila siku ni ngumu kwa raia. Karibu watu milioni tatu wanaishi katika eneo la mgogoro. Ripoti hiyo inaonyesha, hasa, matatizo katika upatikanaji wa huduma za afya, makazi kwa taratibu za kufidiwa kwa vitu na mali viliyoharibiwa, kukamatwa au kuibwa. Mfumo wa cheti kinachoruhusu kuondoka na kuingia kiliotolewa mwezi Januari 2015 na serikali Ukraine kinapelekea kwa hali ya kutengwa.

Hali tete

Kwa upande mwingine wa mstari wa vita, vikosi vya usalama vya Ukraine pia vinanyooshewa kidole, vikituhumiwa kuwazuia watu kinyume cha sheria, mateso na kunyanyaswa. Askari polisi wanaotenda maovu hayo wanaonekana kutoadhibiwa, ripoti imebaini. Uchunguzi kuhusu tuhuma dhidi ya askari polisi hao haufanyiki. Umoja wa Mataifa umebaini kwamba silaha na wapiganaji kutoka Urusi wameendelea kuingia kwa wingi katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi waliojitenga, jambo ambalo linasababisha hali kuwa tete mno. Mapigano mapya yatahatarisha usalama wa watu 800,000 wanaoishi katika katika maeneo hayo mawili yaliyojitenga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.