Pata taarifa kuu

Italia: Wanne wafariki baada ya mlipuko katika kiwanda cha kuzalisha umeme

Mlipuko huo uliotokea siku ya Jumanne, Aprili 9 alasiri katika kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya maji katikati mwa Italia umesababisha vio vya watu wann na watatu kujeruhiwa, na watu watano hawajulikani walipo, manispaa ya mji wa Bologna imesema.

Mji mkuu wa Italia, Roma.
Mji mkuu wa Italia, Roma. AP - Gregorio Borgia
Matangazo ya kibiashara

"Inaonekana sakafu meporomoka na shughuli ya uokoaji ni ngumu kwa sababu maji mengi yamepenya ndani ya ghorofa ya nane ya chini ya ardhi," amesema meya wa mji jirani wa Camugnano, Marco Masinara.

Wafanyakazi wahamishwa

Kampuni ya Italia ya Enel Green Power, kampuni tanzu inayojishughulisha na nishati mbadala ya Enel, inabaini katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa na vyombo vya habari vya ndani kwamba "moto ulizuka na kuathiri transfoma ya kiwanda cha kuzalisha umeme", na kuhakikisha kwamba "hatua zote za usalama" zilifanyika haraka ili kuwezesha "uhamisho sahihi wa wafanyakazi" kwenye eneo la tukio.

Msemaji wa Enel kisha amefafanua kuwa bwawa halikuharibiwa na mlipuko lakini uzalishaji wa nishati ulikatizwa, bila hii kuwa na athari kwa "usambazaji wa umeme katika viwango vya ndani  na katika ngazi ya taifa.

Kulingana na mkuu wa kikosi cha zima moto cha Bologna, Calogero Turturici, aliyehojiwa na televisheni ya ndani, haiwezekani mara moja kuamua sababu za ajali hii. Majengo ambayo mlipuko huo ulitokea yamejaa maji kwa kiasi na kujaa moshi na kwa hivyo hayafikiki mara moja, ameongeza.

"Tunafuatilia matukio katika suala hili kwa wasiwasi," Naibu Waziri Mkuu Antonio Tajani amejibu kwenye ukurasa wake wa X.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.