Shirika la misaada nchini Ufaransa linahofu kuelekea Michezo ya Olimpiki
Shirika la kujitolea kuhusu maji nchini Ufaransa, limetoa tahadhari kuhusu uchafuzi wa mazingira katika mto Seine, wakati huu zikiwa zimebaiki siku 100 kabla ya kuanza kwa michezo ya Olimpiki, mto huo ukitarajiwa kutumika na waogeleaji.
Imechapishwa:
Surfrider Foundation imesema ilikuwa imechambua vipimo vya miezi sita wakati wa msimu wa baridi vilivyofanywa maabara na ikahitimisha kuwa maji ya mto huo yalisalia kuwa machafu na hatari.
Katika barua yake ya wazi, shirika hilo limesema lilitaka kuwashirikisha wadau kwa kuonesha wasiwasi wake kuhusu usalama wa maji yah mto Seine lakini pia hatari zitakazowakabili wanamichezo watakaotumia maji yake.
Mamlaka za jiji la Paris ziko katika shinikizo la kukimbizana na muda kuusafisha mto huo kabla ya kuanza kwa Olimpiki Julai 26, huku njia hiyo maarufu ya maji ikitarajiwa kuwa mhimili wa michezo ya majini.
Takriban euro bilioni 1.4 (dola bilioni 1.5) zimetumika kuboresha miundombinu ya maji taka na maji mfano wa dhoruba ili kupunguza kiwango cha kinyesi kisichotibiwa kinachotiririka kwenye mto huo.
Hata hivyo mamlaka zimetupilia mbali ripoti hii mpya zikisema maji yam to huo yanaelekea kuwa salama kwa binadamu.