Pata taarifa kuu

Ujerumani yahalalisha bangi kwa matumizi ya burudani

Nairobi – Ujerumani imekuwa nchi kubwa ya Umoja wa Ulaya kuhalalisha bangi kwa kwa matumizi ya burudani licha ya pingamizi kali kutoka kwa wanasiasa wa upinzani na wanaharakati wa masuala ya afya wanaosema hatua hiyo itaongeza matumizi yake miongoni mwa vijana.

Raia wa Ujerumani wameonekana kuridhishwa na hatua hiyo.
Raia wa Ujerumani wameonekana kuridhishwa na hatua hiyo. AP - Ebrahim Noroozi
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo ina maana kwamba watu wenye umri wa zaidi ya miaka 18 sasa wanaruhusiwa kubeba gramu 25 za bangi kavu na kulima hadi mimea mitatu ya bangi katika makaazi yao.

Aidha, hii inamaanisha kuwa bangi sio marufuku nchini Ujeremani na hii ni habari njema kwa watumiaji wanaokadiriwa kufikia Milioni 4.5.

Wizara ya afya inasema hatua hii itasaidia kuzuia masoko yasiyo rasmi yanayouzwa bangi, yanayozalisha Euro Bilioni 4 kila mwaka.

Hatua hiyo imepokea pingamizi kali kutoka kwa wanasiasa wa upinzani na wanaharakati wa masuala ya afya.
Hatua hiyo imepokea pingamizi kali kutoka kwa wanasiasa wa upinzani na wanaharakati wa masuala ya afya. AP - Ebrahim Noroozi

Kuanzia Julai mosi, watu wazima wataruhusiwa kununua bangi kutoka kwa vilabu vya watu wasiozidi mia tano ambao kila mmoja atapata hadi gramu hamsini za bangi kila mwezi.

Hata hivyo wanaharakati wa afya wanapinga  hatua hiyo kwa msingi kuwa matumizi ya bangi miongoni mwa vijana yataathiri mfumo wa maisha kwa watumiaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.