Pata taarifa kuu

Urusi yashambulia mitambo mitatu ya nishati ya nyuklia nchini Ukraine

Mitambo mitatu ya nishati ya nyuklia nchini Ukraine imeharibika baada ya kushambuliwa kwa makombora ya ndege zisizo na rubani za Urusi, shirika la kutoa nishati la Ukraine DTEK limetangaza siku ya Ijumaa. "Wavamizi wameshambulia mitambo mitatu ya nishati ya DTEK. Vifaa viliharibiwa vibaya. Baada ya shambulio hilo, wahandisi wameanza haraka kukabiliana na changamoto," DTEK imesema katika taarifa.

Kinu cha nyuklia cha Zaporizhia kwa mara nyingine tena kinazalisha umeme kwa mahitaji ya Ukrainele 27 août 2022
Kinu cha nyuklia cha Zaporizhia kwa mara nyingine tena kinazalisha umeme kwa mahitaji ya Ukrainele 27 août 2022 © AFP
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Urusi limezindua wimbi jipya la mashambulizi ya anga usiku wa kuamkia siku ya Ijumaa, ambayo Paris inalaani. Takriban makombora zaidi ya mia moja na ndege zisizo na rubani zilitumika, kulingana na Ukraine.

Mashambulizi ya Urusi yameharibu 'vibaya' vinu vitatu vya nishati ya nyuklia nchini Ukraine usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa, kujeruhi watu sita na kusababisha kukatika kwa umeme katika baadhi ya maeneo, mamlaka ya Ukraine imesema, ikiishutumu Moscow kwa mashambulio "ya kinyama" dhidi ya mtandao wa nishati yao. Vikosi vya anga vya Ukraine, kwa upande wao, vimesema vimeharibu idadi kubwa ya makombora na ndege 99 zisio na rubani za Urusi - idadi kubwa sana - iliyorushwa wakati wa wimbi hili jipya la milipuko ya usiku.

Moscow imezidisha mashambulizi yake ya anga dhidi ya Ukraine katika wiki za hivi karibuni, hasa ikilenga miundombinu ya nishati, hasa katika kukabiliana na mashambulizi ya Ukraine katika mikoa ya mpaka wa Urusi.

Uhalifu wa kivita unaowezekana

Kwa jumla, mikoa kumi nchini kote ililengwa na watu sita, ikiwa ni pamoja na mtoto, walijeruhiwa, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ukraine imesema.

Ufaransa ilishutumu siku ya Ijumaa mashambulio ya Urusi ambayo yaliharibu vinu vitatu vya nishati yanyuklia nchini Ukraine, ikisema kwamba "yanawezekana kujumuishwa kwa uhalifu wa kivita". "Mashambulizi ya Urusi yaliyolenga maeneo ya uzalishaji wa nishati katika mikoa ya Dnipropetrovsk, Poltava, na Cherkassy yanathibitisha kwamba Moscow inaendelea na mkakati wake wa ugaidi," imesema Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa. "Tunapongeza ujasiri wa Ukraine," Quai d'Orsay pia ilmesisitiza, ikongeza kwamba Ufaransa na washirika wake wataendelea kuunga mkono Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.