Pata taarifa kuu

Urusi: Watu zaidi ya 60 wameuawa katika shambulio la watu wenye silaha

Nairobi – Watu zaidi ya 60 wameuawa wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa baada ya watu wenye silaha kutekeleza shambulio la risasi katika jumba la tamasha jijini Moscow, mamlaka imethibitisha mapema leo Jumamosi, huku kundi la Islamic State likidai kuhusika.

kundi la Islamic State limekiri kuhusika na shambulio hilo.
kundi la Islamic State limekiri kuhusika na shambulio hilo. © Yulia Morozova / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zinawaonyesha watu wenye silaha wakiingia ndani ya ukumbi tamasha kabla ya kufyatua risasi kuelekea walipokuwa watu.

Shambulio hilo lilitokea kabla ya kuanza kwa tamasha la Picnic, bendi maarufu ya rock ambayo hapo awali ilisema kwenye kupitia mtandao wake wa Instagram kuwa ilikuwa imeuza tiketi zote za tamasha hilo.

Rais Putin amewatakia waliojeruhiwa ahueni ya haraka kwa mujibu wa Kremlin
Rais Putin amewatakia waliojeruhiwa ahueni ya haraka kwa mujibu wa Kremlin © Sergei Vedyashkin / AP

Kwa mujibu wa taarifa ya vyombo vya habari vya ndani, tiketi 6,200 za tamasha hilo zilikuwa zimeuzwa ila hadi tukichapisha taarifa hii haikuwa wazi ni watu wangapi walikuwa ndani ya ukumbi wakati wa shambulio hilo.

Shambulio hili limekuja ukiwa imepita wiki mbili tangu ubalozi wa Marekani mjini Moscow kutoa tahadhari ya usalama baada ya kupokea ripoti kuwa watu wanaodaiwa kuwa wenye itikadi kali walikuwa na mipango ya kushambulia mikusanyiko mikubwa mjini Moscow, zikiwemo kumbi za tamasha.

Shambulio hilo limekuja wiki chache tangu Marekani kuonya kuwa watu wenye silaha walikuwa wanapanga kutekeleza shambulio
Shambulio hilo limekuja wiki chache tangu Marekani kuonya kuwa watu wenye silaha walikuwa wanapanga kutekeleza shambulio AP - Sergei Vedyashkin

Waziri wa afya wa Urusi Mikhail Murashko amesema watu 115 wamelazwa hospitalini, wakiwemo watoto watano, mmoja wao akiwa katika hali mbaya. Kati ya wagonjwa 110 watu wazima, 60 walikuwa katika hali mbaya.

Rais Putin ambaye aliarifiwa kuhusu shambulio hilo kulingana na Kremlin aliwatakia ahueni ya haraka majeruhi waliojeruhiwa, naibu waziri mkuu Tatyana Golikova alinukuliwa mashirika ya habari ya Urusi.

Putin hajazungumza hadharani kuhusu shambulio hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.