Pata taarifa kuu

Gaza: Rasimu ya azimio la Marekani katika Umoja wa Mataifa, Blinken ziarani nchini Misri

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema Marekani imewasilisha rasimu ya azimio kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inayotaka "kusitishwa mara moja kwa mapigano yanayohusiana na kuachiliwa kwa mateka" katika Ukanda wa Gaza, katika mahojiano na vyombo vya habari vya Saudia Al Hadath.

Moshi mwingi ukipanda juu ya Gaza baada ya shambulio jipya la Israeli, Machi 14, 2024.
Moshi mwingi ukipanda juu ya Gaza baada ya shambulio jipya la Israeli, Machi 14, 2024. Β© Amir Cohen / Reuters
Matangazo ya kibiashara

"Kwa kweli tuliwasilisha azimio ambalo sasa liko mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa kwa mapigano mara moja kuhusiana na kuachiliwa kwa mateka na tunatumai sana kwamba nchi zitaunga mkono," amesema Antony Blinken, kwenye vyombo vya habari vya Saudi Arabia vya Al Hadath Jumatano usiku Machi 20, kando ya ziara ya nchini humo kuhusu vita kati ya Israeli na Hamas. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ameongeza kuwa anatumai kwamba mpango huu utatuma "ishara kali". Hata hivyo, hakuna kura iliyoratibiwa kwa sasa kwenye rasimu hii. Marekani imepiga kura ya turufu maazimio kadhaa ya kutaka kusitishwa mara moja kwa vita kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas.

Nakala ya azimio hilo, ambalo shirika la habari la AFP limepata kiopi, inasisitiza "haja ya usitishaji vita wa mara moja na wa kudumu ili kulinda raia kutoka pande zote, kuwezesha utoaji wa misaada muhimu ya kibinadamu" na "inaunga mkono bila shaka juhudi za kidiplomasia za kimataifa kufikia usitishaji huo wa mapigano kuhusiana na kuachiliwa kwa mateka ambao wanashikiliwa.

Mwezi wa sita wa vita

Katika mwezi wa sita wa vita vilivyoanza tarehe 7 Oktoba kwa shambulio la umwagaji damu la kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas katika ardhi ya Israel, wasiwasi wa kimataifa unaongezeka kutokana na tishio la njaa na maafa ya binadamu ambayo yanaendelea kuongezeka huko Gaza na zaidi ya vifo 31,923, kulingana na ripoti siku ya Jumatano kutoka Wizara ya Afya ya Hamas. Mapema Machi 21, wizara ilitangaza vifo vya watu wengine 70 kufuatia mapigano ya Israel katika Ukanda wa Gaza ambapo mashahidi wameripoti mashambulizi ya anga ya usiku katikati ya eneo hilo na mapigano makali karibu na hospitali ya al-Shifa huko Gaza (kaskazini).

Kwa ziara yake ya sita Mashariki ya Kati tangu kuanza kwa vita, Bw. Blinken anatarajiwa Alhamisi hii nchini Misri na Machi 22 nchini Israel; atajadiliana na wenyeji wake kuhusu juhudi zitakazofanywa kufikia "makubaliano ya kusitisha mapigano mara moja yanayohakikisha kuachiliwa kwa mateka wote", pamoja na "kuimarishwa kwa juhudi za kimataifa zinazolenga kuongeza misaada ya kibinadamu kwa Gaza na uratibu wa baada ya vita.

Kuepuka mashambulizi ya ardhini dhidi ya Rafah

Marekani mbayo ni mshirika wa kihistoria wa Israel, inajaribu kuepusha mashambulizi makubwa ya ardhini kwenye Rafah, mji unaokaribiana na mpaka uliofungwa wa Misri, ngome kuu ya mwisho ya Hamas, ambapo Wapalestina milioni 1.5 wamejazana, sehemu kubwa ya wakimbizi katika maeneo mengine ya eneo hilo. Hata hivyo, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu anaona operesheni katika Rafah ni muhimu kufikia lengo lake la "kushinda" Hamas na kuizuia kuishambulia Israel tena kutoka Ukanda wa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.