Pata taarifa kuu

Raia wa Urusi wanashiriki katika uchaguzi wa urais

Nairobi – Nchini Urusi, wapiga kura kwa siku tatu kuanzia leo, wanashiriki kwenye uchaguzi wa urais, unaotarajiwa kumpa Vladimir Putin nafasi nyingine ya kuongoza taifa hilo kwa miaka sita zaidi.

Uchaguzi huu unafanyika wakati huu Urusi ikiwa kwenye vita na jirani yake Ukraine kwa mwaka wa tatu sasa
Uchaguzi huu unafanyika wakati huu Urusi ikiwa kwenye vita na jirani yake Ukraine kwa mwaka wa tatu sasa REUTERS - Stringer
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu unafanyika wakati huu Urusi ikiwa kwenye vita na jirani yake Ukraine kwa mwaka wa tatu sasa.

Kuanzia leo mpaka Jumapili, mamilioni ya wapiga kura wanatarajiwa kupiga kura, ambapo Putin mwenye umri wa miaka 71, anakabiliwa na wagombea wengine watatu.

Hata hivyo, wachambuzi wa siasa za Urusi wanasema itakuwa ni vigumu kumshinda Putin, ambaye ambaye amehakikisha kuwa wagombe wake wakuu wamefungwa jela au kukimbia nchi.

Mpinzani wake mkuu Alexei Navalny, alipoteza maisha hivi karibuni akiwa gerezani.

Aidha, wachambuzi wanasema hakuna matumaini kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na haki na rais Putin anatarajiwa kupata ushindi mkubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.