Pata taarifa kuu

G7 yatoa wito kwa Urusi 'kufafanua kikamilifu mazingira' ya kifo cha Alexeï Navalny

Kundi la mataifa saba yaliyostawi zaidi kiviwanda, G7, limeitaka Urusi Jumamosi jioni "kufafanua kikamilifu mazingira" kuhusu kifo cha kiongozi wa upinzani nchi Urusi Alexei Navany, ambaye "alijitolea maisha yake kupigana dhidi ya ufisadi wa Kremlin na kwa uchaguzi huru na wa haki".

Watu wanahudhuria mkutano nje ya ubalozi wa Urusi kufuatia kifo cha kiongozi wa upinzani wa Urusi Alexei Navalny, huko Berlin, Ujerumani, Februari 18, 2024.
Watu wanahudhuria mkutano nje ya ubalozi wa Urusi kufuatia kifo cha kiongozi wa upinzani wa Urusi Alexei Navalny, huko Berlin, Ujerumani, Februari 18, 2024. REUTERS - ANNEGRET HILSE
Matangazo ya kibiashara

"Pia tunatoa heshima usiokuwa wa kifani kwa Alexei Navalny," wamesema viongozi wa G7 (Marekani, Japan, Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Italia, Canada) katika taarifa ya pamoja baada ya mkutano wa kilele kwa njia ya video chini ya uongozi wa Italia.

Baada ya majuma mawili ya mvutano na mamlaka ya Urusi, hatimaye mamake Alexeï Navalny ameweza kupokea mwili wa mwanawe. Tangazo hilo lilitolewa kwenye mitandao na timu ya wapinzani, ambayo imefafanua kuwa bado haijajua ni wapi na chini ya mazingira gani mazishi ya Bwana Navalny yatafanyika.

Kulingana na msemaji wa kiongozi huyu wa upinzani, Lyoudmila Navalnaïa bado yuko Salekhard kuchukua mwili wa mtoto wake. Lakini katika hatua hii, Kira Yarmish amefafanua kwamba bado hajui ikiwa viongozi watazuia mazishi kufanyika kama familia inavyotaka na kama Alexei Navalny anastahili.

Siku mbili zilizopita, Lyoudmila Navalnaïa alirusha video mitandaoni akishutumu uhuni unaofanywa na mamlaka. Alibaini kwamba walitaka kumkabidhi mwili wake kwa sharti tu kwamba mazishi ya mwanawe yafanyike kwa siri.

Bado hakuna habari iliyovuja juu ya uwezekano wa makubaliano kati ya mamlaka na mama wa kiongozi huyo wa upinzani. Mara moja, timu nzima ya Alexeï Navalny, ambayo inaishi uhamishoni nje ya Urusi, inawashukiru kwenye mitandao makumi ya maelfu ya watu ambao walimtolea wito hadharani Vladimir Putin ili mwili wa Bw. Navalny ukabidhiwe familia yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.