Pata taarifa kuu

Heshima ya kitaifa kwa Robert Badinter: 'Jina lako litaandikwa kwenye Pantheon' asema Macron

Ufaransa inatoa heshima ya mwisho kwa Robert Badinter leo Jumatano. Wakili na Waziri wa Sheria wa zamani ambaye alianzisha utaratibu wa kufutwa kwa hukumu ya kifo, ambaye alifariki dunia mnamo Februari 9 na heshima ya kitaifa imefanyika Place Vendome huko Paris, ambapo Wizara ya Sheria inapatikana. "Jina lako lazima liandikwe kwenye Pantheon," Emmanuel Macron amesema wakati wa kumsifu Waziri wa zamani wa Sheria.

Jeneza la Robert Badinter linawasili kwenye Place Vendome huko Paris ambapo Ufaransa inatoa heshima ya mwisho kwa mtu aliyefuta adhabu ya kifo.
Jeneza la Robert Badinter linawasili kwenye Place Vendome huko Paris ambapo Ufaransa inatoa heshima ya mwisho kwa mtu aliyefuta adhabu ya kifo. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

 

Jina la Robert Badinter "lazima liandikwe" katika Pantheon, "pamoja na wale ambao wamefanya mengi kwa ajili ya maendeleo ya binadamu na kwa ajili ya Ufaransa", ametangaza Emmanuel Macron siku ya Jumatano wakati wa wa kutoa heshima za mwisho kwa Waziri wa zamani wa Sheria. "Mnatuacha wakati ambapo wapinzani wenu wa zamani, usahaulifu na chuki, wanaonekana kuendelea tena," ameongeza Rais wa faransa kutoka Place Vendôme, makao makuu ya Wizara ya Sheria ambapo waziri wa zamani wa kisoshalisti aliunga mkono kufutwa kwa adhabu ya kifo. Alimsifu Robert Badinter kama "nguvu inayoishi na kunyakua uhai kutoka kwa mikono ya kifo".

Emmanuel Macron aliahidi kujieleza, katika hotuba yake, juu ya uwezekano wa kuingia kwa wakili, ambaye alifariki wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 95, kwenye Pantheon, hekalu hili au kuba kubwa la jamhuri ambalo linatangaza kwenye msingi wake "Kwa watu wakuu, waliofanya mengi tena makubwa nchini".

Na Robert Badinter alikuwa kweli "mtu mkubwa, alifanya mengi makubwa", rais alikiri siku ya Ijumaa baada ya tangazo la kifo cha waziri wa zamani (1981-1986). "Mambo haya huchukua muda," alisisitiza. "Kwanza ni kwa familia, kwa uhuru, kuchukua muda wanaoona ni muhimu kufanya uamuzi," wasaidizi wa Emmanuel Macron wlieleza siku ya Jumanne.

Eneo la Vendome, mahali pa mfano

Katibu wa kwanza wa chama cha PS, Olivier Faure, alitoa ombi hilo kwa Mkuu wa Nchi. "Ni halali" kwa sababu katika Pantheon ni "watu wakuu ambao walileta mawazo mazuri," amesema siku ya Jumatano kwenye televisheni ya Franceinfo rais wa Baraza la Katiba Laurent Fabius, nafasi iliyoshikiliwa na Robert Badinter kutoka mwaka 1986 hadi mwaka 1995.

Ikulu ya Élysée, kwa kushauriana na familia, walichagua mahali pa ishara kwa kutoa heshima za mwisho kwa Robert Badinter: Place Vendome, ambapo maelfu ya watu wamekuja tangu Jumamosi kutoa heshima kwake. Picha kubwa ya Robert Badinter iliwekwa mbele ya wizara. Hapo ndipo waziri wa François Mitterrand aliandika sheria ya kufuta adabu ya kifo, katika Ufaransa ambayo wakati huo iliunga mkono adhabu kuu.

(Na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.