Pata taarifa kuu

Ufaransa: Serikali imechapisha sheria tata kuhusu uhamiaji

Nairobi – Serikali ya rais Emmanuel Macron imechapisha kwenye gazeti la serikali sheria tata kuhusu uhamiaji siku ya Jumamosi huku maafisa wa idara wakiagizwa kuanza kuitekeleza.

Kabla ya mabadiliko hayo ya sheria hiyo, kulikuwa na maandamano makubwa kulalamikia sheria hiyo
Kabla ya mabadiliko hayo ya sheria hiyo, kulikuwa na maandamano makubwa kulalamikia sheria hiyo © Christian Hartmann / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja siku chache baada ya Mahakama ya Katiba nchini humo kuagiza kufutwa kwa vifungu tata 35 kwenye sheria hiyo.

Miongoni mwa vifungo tata ambayo Mahakama ilisema ni kinyume cha Katiba ni wahamiaji wanaokuja nchini humo kuzuiwa kupata mahitaji muhimu ya kijamii kama kuwawekea mazingira magumu ya kupata ajira.

Hata hivyo, vifungu vya sheria hiyo, vilivyo vingi kama ilivyopendekezwa na serikali hasa kurahihisha mchakato wa kuwafukuza wahamiaji haramu na kuwapa vibali wahamiaji ambao tayari walikuwa kwenye mfumo wa ajira viwandani, viliidhinishwa na Mahakama hiyo.

Kabla ya mabadiliko hayo ya sheria hiyo, kulikuwa na maandamano makubwa kulalamikia sheria hiyo, huku wanasiasa wa mrengo wa kulia, wakiwakosoa Majaji kwa kuharibu sheria hiyo mpya baada ya kuondoa vipengele tata.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.