Pata taarifa kuu

Umoja wa Ulaya wafikia makubaliano kuhusu mageuzi makubwa ya sera ya uhamiaji

Baada ya miaka kadha ya majadiliano na usiku mzima wa mazungumzo ya mwisho, wabunge na wawakilishi wa nchi wanachama wamefikia makubaliano leo Jumatano, Desemba 20, juu ya mageuzi ya tata ya mfumo wa uhamiaji wa Ulaya.

Meli iliyobeba wahamiaji ikikaribia kisiwa cha Sicilia cha Lampedusa, Italia, Septemba 16, 2023.
Meli iliyobeba wahamiaji ikikaribia kisiwa cha Sicilia cha Lampedusa, Italia, Septemba 16, 2023. REUTERS - YARA NARDI
Matangazo ya kibiashara

Mkataba wa Ukimbizi na Uhamiaji utachukua nafasi ya mfumo wa sasa wa Ulaya ambao nchi za kusini mwa Ulaya zimekuwa zikipigia kelele mageuzi kwa angalau miongo miwili. Mkataba huo uliyowasilishwa na Tume ya Ulaya mnamo mwezi wa Septemba 2020, ni jaribio jipya la kurekebisha sheria za Ulaya baada ya kutofaulu kwa pendekezo la hapo awali la mwaka 2016 kufuatia mzozo wa wakimbizi. Kwa ujumla, unatoa udhibiti ulioimarishwa wa wahamiaji wanaowasili katika Umoja wa Ulaya, vituo vilivyofungwa karibu na mipaka ili kurejesha haraka zaidi wale wasio na haki ya kupata hifadhi na utaratibu wa mshikamano wa lazima kati ya nchi wanachama kwa manufaa ya mataifa chini ya shinikizo la Uhamiaji pia inatarajiwa.

Udhibiti ulioimarishwa na utaratibu wa lazima wa mshikamano

Udhibiti wa Dublin unakabidhi jukumu lote la kupokea wahamiaji katika nchi wanakoingia, ambayo kila mhamiaji huwasili katika EU, wakati mwingi kupitia Bahari ya Mediterania, anakumbusha mwandishi wetu huko Brussels, Pierre Bénazet. Mageuzi hayo yanashikilia sheria hii, lakini ili kusaidia nchi za Mediterania, ambako watu wengi walio uhamishoni wanawasili, mfumo wa mshikamano wa lazima unapangwa katika tukio la shinikizo la wahamaji. Mataifa mengine wanachama lazima yachangie kwa kutoa huduma kwa wanaotafuta hifadhi (kuhama) au kwa kutoa usaidizi wa kifedha.

Marekebisho hayo pia yanatoa nafasi ya "kuchuja" kwa wahamiaji wanapowasili na "utaratibu wa mpaka" kwa wale ambao kitakwimu wana uwezekano mdogo wa kupata hifadhi, ambao watawekwa kwenye vituo ili waweze kurejeshwa kwa haraka zaidi katika nchi zao asili au nchi zinakopita. Utaratibu huu utatumika kwa raia wa nchi ambazo kiwango cha utambuzi wa hali ya ukimbizi, kwa wastani katika EU, ni chini ya 20%. Baraza limesisitiza kwamba hata familia zenye watoto chini ya miaka 12 zinapaswa kukabiliwa na utaratibu huo, unaohusisha aina ya kuwekwa kizuizini, katika vituo vilivyo karibu na mipaka au viwanja vya ndege kwa mfano.

"Watu wote wanaoingia katika eneo la Ulaya isivyo kawaida watasajiliwa," anabainisha mbune wa ulaya Fabienne Keller. Tunahitaji kujua ni nani aliye katika eneo letu. Lakini watu hawa pia watakuwa na haki: msaada wa kisheria katika kipindi chote cha hifadhi na ufuatiliaji wa haki za kimsingi ili ziwe za kweli. Kusimamia watu ambao wana nafasi ndogo sana ya kupewa hifadhi kwa haraka zaidi pia ina maana kwamba mifumo yetu ya hifadhi haijasongwa sana na idadi kubwa ya watu wanaosubiri kwa muda mrefu sana. Ina maana ya kuhakikisha kwamba kuna watu wachache waliopo katika taratibu, kwamba wanapokelewa vyema na kuheshimiwa zaidi. »

"Makubaliano ya kihistoria"

Majibu yalikuwa ya haraka. Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen amekaribisha "makubaliano haya ya kihistoria" juu ya Mkataba wa Uhamiaji na Ukimbizi.

Rais wa Bunge la Ulaya, Roberta Metsola kutoka Malta, amesema "anajivunia sana", akiamini kwamba "huenda ilikuwa makubaliano muhimu zaidi ya sheria ya mamlaka hii". Kamishna wa Mambo ya Ndani wa Ulaya Ylva Johansson amepongeza "wakati wa kihistoria".

Ujerumani, mojawapo ya nchi ambazo zimepokea wahamiaji wengi zaidi katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, kwa muda mrefu imetoa wito wa mgawanyo bora wa wakimbizi ndani ya Umoja wa Ulaya, anakumbusha mwandishi wetu wa mjini Berlin, Nathalie Versieux. Kwa hivyo, Kansela Olaf Scholz ameonyesha "unafuu kwa Ujerumani", kwenye mtandao wa X (zamani ikiitwa Twitter). "Kwa hivyo tunazuia uhamiaji haramu na kutoa afueni kwa nchi zilizoathiriwa zaidi, ikiwa ni pamoja na Ujerumani. »Waziri wake wa Mambo ya Ndani Nancy Faeser, pia mwana demokrasia ya kijamii, pia anakaribisha maelewano ambayo yatawezesha kusambaza jukumu la wahamiaji "kwa nchi malimbali".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.