Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Ufaransa: Kile kinachojulikana kuhusu mhusika wa shambulio katika shule ya upili ya Arras

Kijana, mwenye umri wa karibu miaka 20, amewachoma kisu watu kadhaa katika shule ya upili ya Gambetta, katikati mwa jiji la Arras, kaskazini mwa Ufaransa. Mwalimu mmoja amefariki , watu wengine wawili pia wamejeruhiwa. Mshambuliaji huyo aliyekamatwa na polisi, alikuwa chini ya uangalizi wa DGSI na alikaguliwa jana na kukutwa hana kosa lolote.

Maafisa wa polisi na wazima moto walitumwa kwa shule ya upili ya Gambetta-Carnot huko Arras, Oktoba 13, 2023.
Maafisa wa polisi na wazima moto walitumwa kwa shule ya upili ya Gambetta-Carnot huko Arras, Oktoba 13, 2023. © REUTERS/Pascal Rossignol
Matangazo ya kibiashara

Mtu huyo, kulingana na vyanzo vya polisi, alipiga kelele akisema "Allah Akbar" (ikimaanisha Mungu ni Mkubwa) wakati wa shambulio hilo. Ni mtu mwenye asili ya Chechnya, mzaliwa wa Urusi, na ambaye faili yake ilikuwa na herufi S, ambayo ina maana kwamba alikuwa mmoja wa watu wanaotishia usalama wa serikali. Mohammed M., mwenye umri wa miaka 20, alikuwa mwanafunzi wa zamani wa shule hiyo. Kulingana na chanzo cha shirika la habari la AFP, alikuwa akifuatiliwa na Kurugenzi Kuu ya Usalama wa Ndani (DGSI).

"Alikuwa chini ya akifuatiliwa kwa mazungumzo yake ya simu na alikuwa chini ya uangalizi," "tangu majira ya joto," kimesema chanzo hiki, na kuongeza kuwa "mazungumzo yake ya simu hayajafichua, katika siku za hivi karibuni, ushahidi wowote unaomhusisha katika kitendo hiki kibaya."

Ndugu wa mshambuliaji, mwenye umri wa miaka 17, alikamatwa karibu na kituo kingine. Na kulingana na chanzo cha polisi, "wanafamilia kadhaa walikamatwa kwa uchunguzi".

Mwalimu wa falsafa aliyelengwa na mshambuliaji, lakini ambaye alifanikiwa kutoroka - aliambia vyombo vya habari vilivyokuwepo kwenye eneo la tukio kwamba kijana huyo "anatafuta mwalimu wa historia". Mambo ambayo yanakumbusha mazingira ya mauaji ya Samuel Paty, profesa wa historia na jiografia mwenye umri wa miaka 47, aliyekatwa kichwa na kijana mwenye asili ya Chechnya, mnamo Oktoba 16, 2020.

Mwalimu aliyeuawa Ijumaa hii, Oktoba 13 katika shule ya upili ya Gambetta huko Arras alipigwa kisu kwenye koo pamoja na kifuani. Miongoni mwa waliojeruhiwa ni afisa wa shule ya upili aliye katika hali ya dharura kabisa, akiuguza majeraha kadhaa ya kisu, na mwalimu mwingine. Kulingana na chanzo kilicho karibu na faili hiyo, afisa huyo "amejeruhiwa vibaya sana, yuko mahututi". Hakuna mwanafunzi wa shule ya upili aliyejeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.