Pata taarifa kuu

Armenia: Bunge limeidhinisha muswada wa kuwa mwanachama wa ICC

Nchi ya Armenia kupitia bunge, imeidhinisha muswada utakayoifanya nchi hiyo kuwa mwanachama wa mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu wa kivita ICC, hatua iliyoigadhabisha Serikali ya Urusi.

Urusi imelaani hatua hiyo ya Armenia, kujiunga na Mahakama hiyo ambayo imetoa hati ya kukamatwa kwa rais Vladimir Putin
Urusi imelaani hatua hiyo ya Armenia, kujiunga na Mahakama hiyo ambayo imetoa hati ya kukamatwa kwa rais Vladimir Putin AP - Hayk Baghdasaryan
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ni muhimu kwenye mchakato wa Armenia, kujiunga na Mahakama hiyo yenye makao yake mjini Hague, na inakuja baada ya wanajeshi wa Azerbaijani kuendesha operesheni katika jimbo la Nagorno-Karabakh na kupambana na waasi wa Kiarmenia.

Wabunge 60 walipiga kura kuunga mkono nchi hiyo kuwa mwanachama huku wengine 22 wakipinga.

Urusi imelaani hatua hiyo ya Armenia, kujiunga na Mahakama hiyo ambayo imetoa hati ya kukamatwa kwa rais Vladimir Putin.

Moscow inasema hatua hiyo ya Armenia ni kosa, hatua ambayo imesema itaharibu uhusiano kati ya nchi hizo mbili hasa linapokuja kwenye suala la ushirikiano wa masuala ya usalama.

Tangu mwezi Machi, Urusi ilikuwa imeionya Armenia dhidi ya wabunge wake kupiga kura kuunga mkono mkataba wa Mahakama hiyo baada ya kutoa agizo la kukamatwa kwa rais Putin, kwa madai ya kusababisha uhalifu wa kivita nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.