Pata taarifa kuu

Uholanzi: Wawili wauawa katika mashambulizi mawili ya risasi Rotterdam

Watu wawili wameuawa katika mashambulizi mawili ya risasi katika jiji la Uholanzi la Rotterdam, siku ya Alhamisi, Septemba 28,. Shambulio moja lilitokea katika nyumba moja jijini Rotterdam na lingine katika kituo cha hospitali ya chuo kikuu. Msichana mmoja pia amejeruhiwa vibaya. Mshukiwa mwenye umri wa miaka 32 amekamatwa. Sababu za mshambuliaji bado hazijajulikana.

Vikosi maalum vilitumwa Rotterdam baada ya mashamulio mawili ya risasi yaliyosababisha vifo vya angalau watu wawili mnamo Alhamisi Septemba 28, 2023, kulingana na polisi.
Vikosi maalum vilitumwa Rotterdam baada ya mashamulio mawili ya risasi yaliyosababisha vifo vya angalau watu wawili mnamo Alhamisi Septemba 28, 2023, kulingana na polisi. AFP - SEM VAN DER WAL
Matangazo ya kibiashara

Watu wawili waliuawa Alhamisi Septemba 28 kwa kupigwa risasi katika mashambulizi mawili huko Rotterdam, polisi imesema. Mwanaume mwenye silaha amefyatua risasi kwanza katika nyumba moja katika mji wa bandari wa Uholanzi, ambapo alisababisha waathiriwa wawili wa kwanza: mwanamke mwenye umri wa miaka 39 ambaye aliuawa na binti yake wa miaka 14 ambaye amejeruhiwa vibaya.

Kisha akaingia katika hospitali ya karibu ya chuo kikuu, kituo cha matibabu cha Erasme, ambapo alifyatua tena risasi na kumuua mtu mwingine darasani, profesa mwenye umri wa miaka 46. Moto uliwashwa na mshambuliaji katika maeneo yote mawili, lakini uliweza kuzimwa. "Mashambulio mawili ya risasi huko Rotterdam yamesababisha vifo vya watu wawili. Kwanza tutaarifu familia na jamaa na tutatoa maelezo zaidi baadaye,” polisi ya jiji hilo imesema katika taarifa kwenye X (zamani ikiitwa Twitter).

Mshukiwa alikamatwa karibu na kituo cha hospitali

Vikosi vya polisi vilivamia hospitali ya mji wa Uholanzi kumsaka mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye alikuwa amejihami kwa bunduki, mamlaka imesema. Sababu ya shambulio hilo bado haijajulikana, shirika la habari la ANP limesema, likinukuu polisi. Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 32 alikamatwa na polisi karibu na hospitali hiyo na anashukiwa kuwa mhusika pekee wa ufyatuaji risasi, polisi imesema. "Mshukiwa amejulikana na polisi, alikuwa amefunguliwa mashtaka na kuhukumiwa mwaka wa 2011 kwa unyanyasaji wa wanyama," amesema mwendesha mashtaka mkuu wa Rotterdam, Hugo Hillenaar. Polisi pia imesema mshukiwa anashirikiana na wachunguzi.

Picha katika eneo la tukio zimeonyesha watu wakitoka hospitalini, wakiwemo madaktari na wagonjwa, huku maafisa wa polisi wakiwa wamevalia fulana ya kuzuia risasi. Helikopta za polisi ziliruka juu. Madaktari waliovalia makoti meupe walibeba wagonjwa kwenye machela na viti vya magurudumu.

"Kulikuwa na hofu na kulikuwa na kelele nyingi"

Rotterdam mara nyingi ni eneo ambapo hutokea mashambulizi ya risasi, kwa kawaida huhusishwa na suluhu kati ya magenge pinzani ya madawa ya kulevya. Mnamo mwaka wa 2019, watu watatu waliuawa kwa kupigwa risasi kwenye treni za mwendo kasi huko Utrecht, na kusababisha msako mkubwa. Mnamo 2011, nchi ilipigwa  bumbuwazi wakati Tristan van der Vlis mwenye umri wa miaka 24 alipoua watu sita na kuwajeruhi wengine kumi katika jumba la kibiasha lililojaa watu.

(Na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.