Pata taarifa kuu

Ukraine: Shehena ya pili ya nafaka yawasili Istanbul

Kwa mara ya pili, meli ya mizigo ya nafaka kutoka ilitumia ukanda wa baharini uliowekwa na Kyiv ili kuepuka kizuizi kilichowekwa na Urusi. imewasili Jumapili hii, Septemba 24 mjini Istanbul kupitia Bahari Nyeusi, licha ya vitisho vipya vya Moscow kushambulia boti zinazoingia na kutoka Ukraine.

Meli ya mizigo ya Ukraine iliwasili Istanbul ikiwa imesheheni nafaka.
Meli ya mizigo ya Ukraine iliwasili Istanbul ikiwa imesheheni nafaka. © SERGII KHARCHENKO / NurPhoto / NurPhoto via AFP
Matangazo ya kibiashara

Meli mpya imetumia ukanda wa baharini uliowekwa na Kyiv kando ya pwani ya Bahari Nyeusi ili kukwepa kizuizi cha Urusi.

Meli aina ya Aroyat, inayopeperusha bendera ya Palau, iliondoka Ijumaa kutoka Chornomorsk, karibu na Odessa. Kulingana na tovuti za Marine Traffic and Vessel Finder, meli hiyo ya mizigo, ambayo inasafirisha tani 17,600 za ngano ya Ukraine kwenda Misri, ilikuwa Jumapili saa 5 saa za Afrika ya Kati kwenye lango la kusini mwa Bosphorus, katika Bahari ya Marmara.

Ilikuwa inaelekea kwenye Mlango wa Bahari wa Dardanelles kufikia Bahari ya Mediterania. Mnamo mwezi Julai, Moscow ilijiondoa kwenye makubaliano ya kimataifa yaliyotiwa saini mnamo Julai 2022, kupata mauzo ya bidhaa za kilimo za Ukraine kupitia Bahari Nyeusi.

Mkataba huu ulifanya iwezekane kuuza nje karibu tani milioni 33 za nafaka katika mwaka mmoja. Meli ya kwanza iliyopakia tani 3,000 za ngano na pia kupeperusha bendera ya Palau iliondoka katika bandari hiyo ya Chornomorsk bila tukio lolote siku ya Jumanne na kuwasili Istanbul siku ya Alhamisi.

Kiev inataka kuanzisha njia za usambazaji bidhaa kwa Afrika ili kukabiliana na ushawishi wa Urusi, ambayo msimu huu wa kiangazi iliahidi baadhi ya mataifa ya Afrika kuyapeleka ngano bila malipo. Urusi na Ukraine ni nchi mbili zinazoendesha kilimo zaidi duniani ambazo uzalishaji wake ni muhimu kwa usalama wa chakula duniani. Uvamizi wa Urusi kwa jirani yake na vikwazo vya kimataifa dhidi ya Moscow vimedhoofisha usambazaji wa bidhaa hiyo na masoko ya kimataifa.

Wanajeshi wa Ukraine pia wamekuwa wakifanya kazi kwa wiki kadhaa kukabiliana na udhibiti wa kijeshi wa Urusi katika Bahari Nyeusi. Kwa hivyo siku ya Jmamosi Kiev ilidai  kuwaua au kuwajeruhi "makamanda waandamizi" kadhaa wa jeshi la wanamaji la Urusi wakati wa shambulio la anga siku ya Ijumaa dhidi ya makao makuu ya kikosi cha wanamaji wha Urusi kwenye Bahari Nyeusi, huko Sevastopol, katika eneo lililounganishwa na Urusi la Crimea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.