Pata taarifa kuu

Ufaransa: Wasambazaji kuuza petroli kwa hasara katika miezi ijayo ili kufidia mfumuko wa bei

Waziri Mkuu wa Ufaransa Élisabeth Borne ametangaza hatua mpya ya kukabiliana na mfumuko wa bei ya mafuta, huku bei zikitishia kuvuka euro mbili kwa lita. Wadau wa biashara ya mafuta wataruhusiwa kuuza petroli "kwa hasara" kwa miezi michache.

Elisabeth Borne ametangaza kuwa wasambazaji wataweza kuuza petroli kwa hasara katika miezi ijayo ili kufidia mfumuko wa bei.
Elisabeth Borne ametangaza kuwa wasambazaji wataweza kuuza petroli kwa hasara katika miezi ijayo ili kufidia mfumuko wa bei. AFP - EMMANUEL DUNAND
Matangazo ya kibiashara

 

Élisabeth Borne ametangaza kwamba waagizaji na wasambazaji wa mafuta wataweza kuuza petroli "kwa hasara" kwa miezi michache ili kuwaruhusu "kupunguza bei zaidi", katika mahojiano yaliyotumwa mtandaoni Jumamosi Septemba 16 kwenye tovuti ya Le Parisien. "Kwa hatua hii ambayo haijawahi kushuhudiwa, tutakuwa na matokeo yanayoonekana kwa Wafaransa, bila kutoa ruzuku ya mafuta," alihakikishia, baada ya kukumbusha kuwa kuuza kwa hasara kumepigwa marufuku na sheria tangu 1963.

Mkuu wa serikali hakukubali mapendekezo ya upinzani ambayo yanataka aidha punguzo kama mwaka mmoja uliopita, au kupunguzwa kwa ushuru wa petroli ili kukabiliana na kupanda kwa bei ya mafuta ambayo imefikia euro mbili kwa lita (2€/L). "Kila mtu anachukua sehemu yake," amebainisha, akisema kuwa "ni kawaida kuwashirikisha wanaviwanda wakubwa", huku akikumbusha kuwa "jukumu la Serikali pia ni kupunguza nakisi yake na deni lake."

Vyama vya vituo vya mafuta vinachukulia hatua hiyo kuwa haiwezekani

Tangazo hili limemshangaza Francis Pousse, kiongozi wa chama cha vituo vya mafuta cha Mobilians ambacho kina vituo vya mafuta 5,800 vya huduma za kitamaduni, bila kujumuisha maduka makubwa. Anasema hatua hii mpya ni jibu kwa maduka makubwa, kuwaruhusu "kupambana" katika sekta hii yenye ushindani mkubwa, wakati bei ya mafuta kwenye masoko ya kimataifa "hivi karibuni itazidi euro 1.99". .

"Sisi, wauza mafuta, hakuna suala la kuuza kwa hasara," ameliambia shirika la habari la AFP. Kabla ya kuongeza: "Wanachama wangu wanaishi kwa 40, 50% au hata zaidi kutokana na uuzaji wa mafuta, kwa hivyo ikiwa watauza kwa hasara, ninawapa miezi mitatu." Katika soko ambalo tayari limebanwa sana, anaonyesha kwamba kiwango cha jumla cha vituo vya jadi ni "senti moja hadi mbili" kwa lita katika nyakati za kawaida.

Bw. Pousse pia anasema "ana shaka" kuhusu athari za hatua hii kwa wanunuzi. Kwa sababu ikiwa bei za wauzaji wa maduka makubwa zitaendelea kuongezeka, "hawataweza kumudu kupoteza senti 15 kwa kila lita ya petroli". Hakuna msambazaji au mwagizaji wa mafuta ametoa maoni yake kufuatia tangazo la mkuu wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.