Pata taarifa kuu

Ufaransa:Marufuku dhidi ya vazi la abaya inaanza kutekelezwa leo.

Wiki iliyopita serikali ya Ufaransa ilitangaza marufuku kwa wanafunzi wa kike katika shule za umma kuvaa vazi aina ya abaya ambayo huvaliwa mara nyingi na wafuasi wa dini ya kiislamu nchini humo.

Vazi la Abaya lapigwa marufuku kwenye shule za serikali nchini Ufaransa.
Vazi la Abaya lapigwa marufuku kwenye shule za serikali nchini Ufaransa. © @Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo ya kutovaa abaya inakuja baada ya Ufaransa kupiga marufuku alama  za kidini katika shule za serikali na hata majengo ya serikali ikisema kuwa zinakiuka sheria za kilimwengu.

Mapema leo mamlaka nchini humo imesema kuwa inazifuatilia  shule takribani 500 mabazo huenda zikakaidi amri hiyo wakati huu shule zinapofunguliwa.Amesema waziri wa Elimu nchini humo Gabriel Attal.

Rais Emmanuel Macron aliweka wazi kuwa wanafunzi watakaovalia mavazi aina ya abaya au buibui hawataruhusiwa kuingia madarasani .Alizungumzia kanuni hiyo ya mavazi kwa mara ya kwanza hadharani baada ya kutembelea shule moja katika eneo la Vaucluse kusini mwa Ufaransa.

Macron amesema anajuwa kutakuwa na visa vya wanafunzi kuijaribu sheria hiyo pamoja na wale watakaojaribu kupinga mfumo huo.

Mwaka 2004  nchi hiyo ilipiga marufuku wasichana kuvaa vazi la Hijab hasaa katika shule zinazomilikiwa na serikali.

Abaya ni vazi refu linalotiririka kama joho linalovaliwa na wanawake wengi wa Kiislamu. Vazi la abaya ambalo linachukuliwa kuwa buibui la mtindo wa kisasa huvaliwa na baadhi ya wanawake wa Kiislamu kama stara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.