Pata taarifa kuu

Urusi: Makundi wanamgambo kulazimika kula kiapo

Siku mbili baada ya kutangazwa kifocha Yevgeny Prigozhin, rais wa Urusi Vladimir Putin ametia saini agizo siku ya Ijumaa Agosti 25 linalowalazimisha wapiganaji wa makundi ya wanamgambo kula kiapo kwa kutetea na kuihami Urusi, kama wanajeshi wa jeshi la serikali wanavyofanya. Hatua mpya ili makundi hay yote yawe imara chini ya uwajibikaji wa serikali ya Urusi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin katika mkutano wa kijeshi huko Moscow, Agosti 24, 2023.
Rais wa Urusi Vladimir Putin katika mkutano wa kijeshi huko Moscow, Agosti 24, 2023. via REUTERS - SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Moscow, Anissa El Jabri

Takriban mwezi mmoja uliopita, agizo la rais liliitaka kampuni yoyote mpya ya kikanda kuwa chini ya mamlaka ya serikalina kuwa na hadhi ya kisheria, na kuundwa kwake "chini ya idhini ya Vladimir Putin".

Wakati huu, agizo la rais linahusu makundi yote ya wanamgambo, ambayo ni mengi nchini Urusi: vikosi mbali mbali vya kujitolea, vikosi vya ulinzi wa taifa, na vile vyote "vinavyochangia katika utekelezaji wa majukumu yaliyopewa vikosi vya jeshi la Urusi" na "na taasisi zingine za kijeshi." 

Wote lazima, kama askari wa jeshi la serikali, hasa kuapa "kutii" na "kutetea na kuihami" Urusi na, kati ya mambo mengine, "kufuata kikamilifu maagizo ya makamanda na maafisa wakuu", na pia "kuheshimu kwa moyo mkunjufu Katiba ya Urusi".

Hii ni mara ya kwanza kwa makundi haya kupewa masharti na majukumu ya kufanya. Na wote watafanya hayo, kwa agizo la Vladimir Putin.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.