Pata taarifa kuu

Joe Biden anasema 'hashangazwi' na uwezekano wa kifo cha Prigozhin nchini Urusi

Rais wa Marekani Joe Biden anasema "hajashangazwa" na uwezekano wa kifo cha bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin katika ajali ya ndege siku ya Jumatano nchini Urusi. 

Joe Biden, akiwa katika milima ya Magharibi mwa Marekani na familia yake, pia amefahamishwa juu ya hali hiyo, Ikulu ya White imesema.
Joe Biden, akiwa katika milima ya Magharibi mwa Marekani na familia yake, pia amefahamishwa juu ya hali hiyo, Ikulu ya White imesema. © AP
Matangazo ya kibiashara

"Sijui kabisa nini kilitokea, lakini sishangai," amewaambia waandishi wa habari.

"Mambo machache hayafanyiki nchini Urusi bila Putin kujua au kuwa na uhusiano wowote," ameongeza rais huyo wa Marekani kutoka milima ya Magharibi mwa Marekani ambako yuko na familia yake.

"Tumeona kile kilichoripotiwa. Ikithibitishwa, haitakuwa jambo la kushangaza kwa mtu yeyote," Adrienne Watson, msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa la serikali ya Marekani, alisema mapema.

"Vita vinavyosabaisha maafa nchini Ukraine vilisababisha jeshi la kibinafsi kuandamana Moscow na sasa - huenda kifo chake kinatokana na - hatua hiyo," aliongeza.

Ndege ya kibinafsi iliyokuwa na watu kumi ilianguka siku ya Jumatano Agosti 23 katika eneo la Tver, Urusi, ilipokuwa ikisafiri  kati ya Moscow na Saint Petersburg, na kuua watu wote waliokuwa ndani, idara ya huduma za dharura ilitangaza, na bosi wa kundi la wanamgambo Wagner Yevgeny Prigojine alikuwa kwenye orodha ya watu hao.

Alikuwa nyuma ya uasi mwezi Juni dhidi ya makao makuu ya jeshi la Urusi na Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu, likiongozwa na wapiganaji wake, ambao waliteka maeneo ya kijeshi kwa muda mfupi kusini mwa Urusi kabla ya kuelekea Moscow.

Vladimir Putin alimwita msaliti, bila kutaja jina lake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.