Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Ufaransa: Maafisa wa polisi wahamishwa baada ya kupokea vitisho vya kigaidi

Maafisa wa polisi kutoka vyuo vitatu vya polisi, huko Nîmes, Saint-Malo na Oissel - Seine-Maritime -, viwalihamishwa usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi baada ya kupokea vitisho vya kigaidi, kimesema chanzo cha polisi kinachofahamu suala hilo. 

Picha ya gwaride la Julai 14, 2018.
Picha ya gwaride la Julai 14, 2018. AFP/Thomas Samson
Matangazo ya kibiashara

"Jana usiku, taarifa zililetwa kwetu zinazotaka kutekelezwa kwa zoezi la kuwahamisha mara moja maafisa wa shule kadhaa za polisi (ENP), ambazo ni Nîmes, Oissel na Saint-Malo", makao makuu ya polisi (DGPN) yamebainisha kwa shirika la habari la AFP. 

DGPN haikubainisha aina ya tahadhari hiyo, lakini, kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na uchunguzi kwa shirika la habari la AFP, ni barua iliyowasilishwa katika chuo cha polisi cha Nîmes ikiwa na vitisho vya kigaidi. "Ukaguzi, uliofanywa kama tahadhari, ulisababisha kuhamishwa kwa maafisa wa polisi ambao walikuwa wamelazwa", anaongeza DGPN imeongeza. "Upelelezi huu, unaosaidiwa na mbwa wa upekuzi, bado unaendelea bila kufichua chochote cha kutilia shaka", kulingana na polisi ya kitaifa. Uchunguzi ulifunguliwa na kukabidhiwa kwa mahakama ya Nîmes.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.