Pata taarifa kuu

Urusi: Polisi yafanya upekuzi kwa shirika kubwa linalofuatilia uchaguzi

Maafisa kadhaa wa shirika lisilo la kiserikali la Golos (“sauti”, kwa Kirusi) linalojihusisha na ufuatiliaji wa uchaguzi, nchini Urusi wamelengwa na upekuzi na afisa mmoja amekamatwa leo Alhamisi Agosti 17, 2023.

Kituo cha kupigia kura wakati wa kura ya maoni iliyoandaliwa na Urusi huko Luhansk, Donbass, Septemba 27, 2022.
Kituo cha kupigia kura wakati wa kura ya maoni iliyoandaliwa na Urusi huko Luhansk, Donbass, Septemba 27, 2022. © AP
Matangazo ya kibiashara

Kutoka kwa mwandishi wetu huko Moscow,

Uchaguzi wa mwisho kabla ya uchaguzi wa urais wa Aprili utafanyika Septemba 10 nchini humo. Huu ni uchaguzi wa magavana. Tarehe 17 mwezi huu wa Agosti, ilikuwa pia siku ya mwisho ya uchunguzi wa wagombea na tume za uchaguzi.

Miaka miwili iliyopita, tena kabla ya uchaguzi - wakati huo ulikuwa ni uchaguzi wa wabunge - shirika hili la Golos liliorodheshwa kama 'afisa wa kigeni'. Uchaguzi uliopita, maafisa wake kadhaa waliwekwa mmoja baada ya mwingine kwenye orodha hii yenye sifa mbaya.

Siku ya Alhamisi, Agosti 17, msako wa polisi ulifanyika katika nyumba za wafanyakazi 14, katika mikoa minane, ikiwa ni pamoja na ile ya Moscow, Kazan na Saint Petersburg. Simu na kompyuta za mratibu wa shirika hili zilikamatwa. Naibu kiongozi wa Golos alikamatwa na kuhojiwa.

Wapinzani kutupwa gerezani au kulazimishwa kukimbilia uhamishoni

Grigori Melkoniants anashukiwa kuhusishwa na shirika linaloelezewa nchini Urusi kama "lisilofaa". Kosa ambalo nchini Urusi, sheria ya jinai hutoa hadi miaka sita jela. Golos ni shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na ufuatiliaji wa uchaguzi na utetezi wa wapigakura linalojulikana kwa kuripoti kwake kwa usahihi na kwa kina kuhusu udanganyifu wa kura.

Tangu kuanza kwa mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine, karibu wapinzani wote wakuu wamefungwa nchini Urusi au kukulazimishwa kwenda uhamishoni nje ya nchi. Maelfu ya raia wa kawaida pia wamefunguliwa mashtaka, hasa kwa kukemea mzozo huo, wengine wamehukumiwa vifungo vizito.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.