Pata taarifa kuu
UTAMADUNI-ULINZI

Vita vya Ukraine: Waziri wa Utamaduni alazimika kujiuzulu

Oleksandre Tkatchenko ametangaza kujiuzulu baada ya "kutoelewana" juu ya matumizi ya fedha za umma kwa miradi ya kitamaduni.

Waziri wa Utamaduni wa Ukraine Oleksandre Tkatchenko amejiuzulu siku ya Ijumaa baada ya "kutoelewana" na rais kuhusu fedha za umma.
Waziri wa Utamaduni wa Ukraine Oleksandre Tkatchenko amejiuzulu siku ya Ijumaa baada ya "kutoelewana" na rais kuhusu fedha za umma. © ANNE-CHRISTINE POUJOULAT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mzozo wa serikali katika kiini cha vita. Waziri wa Utamaduni wa Ukraine ametangaza kujiuzulu mapema Ijumaa Julai 21 baada ya "kutoelewana" juu ya matumizi ya fedha za umma kwa miradi ya kitamaduni, huku Kyiv ikijaribu kuzuia uvamizi wa Urusi.

"Nimewasilisha barua yangu ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu (Alhamisi) jioni, kutokana na kutoelewana kuhusu umuhimu wa utamaduni wakati wa vita", aeandika Oleksandre Tkatchenko kwenye Telegram. "Wakati wa vita, fedha za kibinafsi na za kibajeti kwa utamaduni sio muhimu sana kuliko ndege zisizo na rubani, kwa sababu utamaduni ndio ngao ya utambulisho wetu na mipaka yetu," ameongeza, bila kutoa maelezo zaidi juu ya sababu za kujiuzulu.

Siku ya Alhamisi jioni rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitoa wito wa uteuzi wa waziri mpya wa utamaduni, akikosoa matumizi ya bajeti ya serikali kwa miradi ya kitamaduni kwa kudhoofisha ulinzi. "Wakati wa vita kama hii, serikali inakuwa makini, na hivyo kutumia rasilimali za serikali kwa ulinzi," Volodymyr Zelensky alisema katika hotuba yake ya kila siku.

Euro milioni kumi na moja zatengwa kwa ajili ya utengenezaji wa vipindi vya televisheni

"Makumbusho, vituo vya kitamaduni, alama, mfululizo vipind vya televisheni - yote haya ni muhimu, lakini sasa kuna vipaumbele vingine. Tafuteni pesa za ziada. Si fedha za serikali,” aliongeza Volodymyr Zelensky, akibaini kwamba alimwomba Waziri Mkuu Denys Chmygal kumteua wazizi mpya kuchukua nafasi ya Oleksandre Tkatchenko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.