Pata taarifa kuu

Iran:Watu wawili wanyongwa kwa kosa la kukufuru.

Nairobi – Nchi ya Iran mapema leo imewanyonga wanaume wawil Sadrollah Fazeli Zare na Youssef Mehrdad baada ya kukutwa na hatia ya kumtusi Mtume Mohammad na kuichoma Kurani.

Wanaume wawili wanyongwa nchini Iran
Wanaume wawili wanyongwa nchini Iran © REUTERS/Michele Tantussi
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mahakama hiyo ni kuwa Machi 2021, mmoja wa washtakiwa alikiri kuchapisha maudhui  hayo kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii.

Wawili hao pia walishutumiwa kwa kumiliki  akaunti  za mitandao ya kijamii na vikundi ambavyo vinaendeleza ukafiri na kudhalilisha dini ya Kiislamu.Liliripoti shirika la habari la mahakama ,Mizan.

Mizan lilisema kuwa Sadrollah Fazeli-Zare na Yousef Mehrad walinyongwa katika gereza la Arak Prison lililopo katikati mwa Iran.

Kulingana na mashirika ya kutetea haki za binadamu ikiwa ni pamoja na Amnesty International ni kuwa Iran inawanyonga watu wengi zaidi kila mwaka kuliko taifa lingine lolote isipokuwa China.

Nchi  ya Iran ilinyongwa asilimia 75 zaidi ya watu mwaka 2022 kuliko miaka uiliyopita, mashirika mawili ya haki za binadamu yalisema mwezi Aprili.

Takriban watu 582 walinyongwa nchini Iran mwaka jana, idadi kubwa zaidi ya watu walionyongwa nchini humo tangu 2015 na zaidi ya 333 walionyongwa mwaka 2021, kundi lenye makao yake makuu nchini Norway la Iran Human Rights (IHR) na lenye makao yake mjini Paris la Together Against the Death Penalty. (ECPM) ilisema katika ripoti ya pamoja.

Siku ya Jumamosi, Iran ilitekeleza hukumu ya kunyongwa kwa mpinzani wa Uswidi na Iran Habib Chaab kwa "ugaidi", na kukemewa vikali na Uswidi na Umoja wa Ulaya.

Wakati huo huo, Mjerumani-Irani Jamshid Sharmahd, 68, anahukumiwa kifo na Iran, ambayo haitambui utaifa wa nchi mbili, kuhusiana na shambulio mbaya la msikiti mnamo 2008.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.